BREAKING

Friday 27 January 2017

SERIKALI YAWAFUNGULIA SIMBA, UWANJA WA TAIFA SASA KUANZA KUTUMIKA KESHO,AZAM FC KUKIPIGA NA SIMBA TAIFA

SERI


Serikali imeufungulia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na imeruhusu mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC na Simba uchezwe hapo kesho.

Simba watakuwa wenyeji wa Azam FC kesho katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mchezo huo utafanyika rasmi Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru, Dar es Salaam kufuatia tamko la Serikali .

Afisa Habari wa Simba Hajji Manara amedhibitisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya soka Tanzania TFF ambapo amesema kuwa Serikali imewaachia kuutumia Uwanja wa taifa akisema ni jambo jema na linaonyesha nia njema ya kukuza soka nchini.

Amewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuzingatia nidhamu ndani ya uwanja huo, kwani iwapo mwanachama na shabiki yoyote atafanya jambo kinyume na maadili atachukuliwa hatua kali kwa kuwa sasa uongozi wa klabu umeamua kulivalia njuga suala la nidhamu kwa mashabiki.

Taaruifa za awali zilizotolewa na Zawadi Msalla, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali zimesema kwamba Uwanja huo unafunguliwa baada ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kujiridhisha na ukarabati uliofanywa baada ya uharibifu uliosababishwa na tukio la Oktoba 1, mwaka jana kati ya mechi ya Simba na Yanga iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo kulitokea vurugu baina ya mahasimu,hao na kuvunja viti, baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu.

Tambwe alifunga bao lake dakika ya 26, akimalizia pasi ya beki Mbuyu Twite na kufunga lakini mashabiki hawakukubaliana na bao hilo baada ya wachezaji wa Simba kumvaa mwamuzi Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.

Katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa madai ndiye aliyekuwa mstari wa mbele, kuleta vurugo, ambapo baadae Mkude alifutiwa kadi hiyo na Saanya kufungiwa miaka miwili kuchezesha.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube