BREAKING

Thursday, 5 January 2017

KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MONDULI, LEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo ameongoza mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Jacob Nkomola, yaliyofanyika Mtoni Kijichi, Temeke Dar es Salaam.

Katika mazishi hayo walikuwepo piaa viongozi wengine wa ngazi ya juu wa CCM, wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu. Ngemela Lubinza.

Nkomola ambaye alifariki juzi jijini Dar es Salaam, mwili wake ulitangulia kuagwa nyumbani kwake, Mtoni Kijichi na baadaye kupelekwa katika Kanisa la Kianglikana, Mtoni Kijichi kabla ya kuzikwa katika makaburi yaliyopo Kijichi  saa kumi jioni. 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube