Tottenham imefutilia mbali ndoto ya
Chelsea kutaka kuweka historia katika ligi kuu ya England kwa kushinda
michezo 14 baada ya vinara hao kuchakazwa 2-0 White Hart Lane.
Spurs
wamekwaa mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi baada ya Dele Alli
kufunga magoli yote mawili kwa njia ya kichwa hii ikiwa ni mwishoni mwa
kipindi cha kwanza na dakika ya 54.Alli alifunga vyema kwa kupokea pasi safi kutoka kwa Christian Eriksen kwa magoli yote mawili.
Eden Hazard alikuwa na nafasi mbili za kuiokoa Chelsea lakini Spurs waliweza kufanikiwa kupata alama tatu muhimu na kuwaondoa majirani zao Arsenal katika nafasi ya nne
No comments:
Post a Comment