BREAKING

Saturday, 21 January 2017

SERIKALI YAMPONGEZA MWANARIADHA ALPHONCE FELIX SIMBU KWA KUILETEA SIFA TANZANIA KWENYE RIADHA

 Mwanariadha Alphonce Felix Simbu akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na wadhamini wake DSTV
 Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Wilhelm Gidabuday 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza katika hafla ya kumpongeza mwanariadha Alphonce Felix Simbu baada ya kutwaa ubingwa katika mashindano ya Riadha Mumbai-India

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanazania  Baraka Shelukindo akitoa nemno katika hafla hiyo,DSTV ni wadhamini wa Simbu.

Serikali imempongeza mwanariadha kimataifa Alphonce Felix Simbu kufuatia ujasiri wake kufuatia ubingwa wa mbio za Marathoni kwa mwaka huu nchini India.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nanuye wakata wa hafla maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Multi-Choice Tanzania jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na pongezi amemshukuru kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania  katika medani za kimataifa.

Aidha Waziri Nape pia ameipongeza kampuni ya Multichoice Tanzania kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha sekta ya michezo inapiga hatua, huku uongozi wa kampuni hiyo ukiahidi kuendelea kumdhamini mwanariadha huyo katika ushiriki wake kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa.

Kwa upande wao, bingwa Alphonce Simbu na Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Wilhelm Gidabuday pamoja na kuishukuru Serikali wamewaomba wadau wa michezo kuwaunga mkono wanariadha wengine jambo litakalosaidia kutengeneza timu bora kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube