Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Seif Suleman akiwa katika bandari ya Zanzibar kuupokea Ujumbe wa Madaktari kutoka Jumuiya ya Watanzania Washington ukiwa wenyeji wa PBZ na Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora Zanzibar wakiwa katika bandari hiyo kuupokea kwa ajili ya kutoa huduma ya Afya kwa Wananchi wa Zanzibar katika hospitali ya Mnazi mmoja kesho, Kwa muji wa Mkurugenzi wa Idara hiyo Ndg Adila Hilal Vuai amesema utatoa huduma ya Uchunguzi wa Satatani ya Maziwa kwa Kinamama, Kisukari, Presha Meno na tiba nyengine kwa wananchi wa Zanzibar watakaofika katika hospitali hiyo kupata huduma hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa PBZ Ndg Seif Suleiman akisalimiana na mmoja wa madaktari hao Bingwa walipowasili katika bandari ya forodhani wakitokea Dar -es- Salaam walikuwa wakitowa huduma hizo kwa Wananchi.katikati Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Ndg Adila Hilal Vuai. wakiwapokea wageni wao.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washington Ndg Iddi Sandaly akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBA) Ndg Seif Suleiman alipowasili katika bandari ya Zanzibar wakitikea Dar na Ujumbe wa Madaktari 17 watakuwa Zanzibar kwa kutoa huduma ya Tiba kwa Wananchi wa Zanzibar katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kesho asubuhi.
Madktari kutowa Washington DC,MD,VA wakiwasili katika bandari ya Zanzibar wakitokea Dar-es-Salaam baada ya kutoa huduma ya Tiba.kwa Wananchi wa Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Diaspora Zanzibar Ndg Adila
Hilal Vuai akiwa na mmoja wa Madaktari hao Dr. Hailu wakizungumza wakati
alipowasili katika bandari ya Zanzibar jioni hii tayari kwa kutowa
huduma ya matibabu kwa Wananchi wa Zanzibar katika hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja kesho. wakitoka katika bandari ya Zanzibar. Madaktabi
Bingwa wakifurahia mandhari ya Zanzibar wakiwa katika bandari ya
Malindi Zanzibar baada ya kuwasili katika Visiwa vya Marashi ya Karafuu. Kwa hisani ya ZanziNews
Watanzania wanaoishi Washinton Bi Asha Nyanganyi akiwa na Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washinton Ndg Iddi Sandaly.wakiwa katika bandari ya Zanzibar walipowasili leo jioni wakitokea Dar,
No comments:
Post a Comment