Wachezaji wa Azam FC Didier Kavumbagu,Erasto Nyoni,Wawa na Himid Mao wakishangilia bao lao lililofungwa na mshambuliaji John Bocco.
Mfungaji wa bao la ushindi dhidi ya KCC ya Uganda John Bocco akishangilia
Na Said Makala
TIMU Azam FC imeanza vyema michuano ya kombe la Kagame baada ya kuifunga KCC ya Uganda bao 1-0.
Bao pekee la Azam fungwa na mshambuliaji John Bocco ambaye pia ni mchezaji wa Taifa Stars,bao ambalo lilizamisha jahazi la KCC, Bocco alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Shomari Kapombe ambaye aliambaa ambaa na mpira upande wa kulia na kumimina krosi safi iliofika katika miguu ya Bocco aliyewalima chenga mabeki wa KCC na kufunga kwa ulaini.
Azam waliendelea kulisakama lango la KCC, lakini umakini wa washambuliaji Didier Kavumbagu, na Bocco ulikuwa mdogo kwani walikosa mabao ya wazi, kipindi cha pili Bocco alishindwa kutumia kwa mara nyingine krosi safi ya Kipre Tcheche, baada ya kubaki yeye na nyavu huku kipa akiwa ameenda malikiti, lakini alipiga shuti kali lililoenda nje.
Hadi dakika 90 zinamalizika Azam waliibuka na ushindi huo na kujiweka vyema katika kinyang'anyiro cha michuano hiyo.

No comments:
Post a Comment