BREAKING

Thursday, 30 July 2015

NISHATI YA GESI ASILIA KUTUA DAR MWEZI UJAO

Baadhi ya Mitaambo ya Gesi asilia

 

Jitihada za serikali katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa umeme nchini, sambamba na matumizi ya nishati ya gesi asilia, kwa ajili ya kufulia mitambo ya umeme hatimaye vimekamilika.

Kuanzia mwezi ujao uzalishaji umeme kwenye mradi wa Kinyerezi jijini Dar es salaam utaanza kuzalisha megawati 75 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya taifa, baada ya kukamilika kwa asilimia 95 ya mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150.

Wajumbe wa bodi ya shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC wakitembelea miradi ya uzalishaji na uchakataji wa gesi kwenye kiwanda cha Gesi Songosongo pamoja na mitambo ya kufua umeme wa gesi wa Kinyerezi na Tegeta wameelezea kuridhishwa na hatua zilizofikiwa kwenye miradi hiyo iliyoghrami taifa zaidi ya shilingi trilion mbili.

Kuhusiana na kukamilika kwa mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi wenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 150, meneja wa Tanesco toka Mradi wa Kinyerezi 1 anaeleza zaidi.

Mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni wa pili kumilikiwa na Serikali kupitia TPDC kwa asilimia mia moja baada ule mradi wa bomba la gesi kutoka Ubungo mpaka maeneo ya Mikocheni uliozinduliwa tarehe 26 Julai, 2014.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube