BREAKING

Monday, 20 July 2015

DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA AZINDUA KISIMA CHA MAJI SAFI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA WATOTO WETU TANZANIA


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.

DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza katika hafla ya kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na Chief Commerial Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Watoto wa kituo hicho na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Watoto wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akipokea risasi ya watoto wa kituo hicho.
Vijana wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alitoa ahadi ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akifungua pazia wakati akizindua kisima cha maji katika Kituo cha Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana. Kisima hicho kimejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Simu ya Zantel.
DC Makonda akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa kisima hicho.
Hapa DC Makonda akimtwisha maji mmoja wa wanafunzi wa kituo hicho baada ya kukizindua.
DC Makonda akimkabidhi kitabu, mtoto Yusla Omari kwenye uzinduzi huo.
DC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya kituo hicho.

Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Simu ya Zantel jana ilitoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha  upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima hicho kilichokabidhiwa jana kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka

‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano hayo, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.

‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.

Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.

Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.


‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’ alisema Tegete. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube