BREAKING

Wednesday, 8 July 2015

RAIS KIKWETE AJIANDIKISHA KUPIGA KURA KWA KUTUMIA BVR MSOGA


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo .Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.


Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo .


Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.

 Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo
Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo(picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube