BREAKING

Monday 27 July 2015

UKAWA WAMSAFISHA LOWASA, WASEMA NI MSAFI ANAWAFAA, HANA KASHFA YA UFISADI

Khamis

Umoja wa Vyama Vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi -Ukawa vimemtaka na Waziri Mstaafu bw.Edward Lowasa kujiunga na Umoja huo na kuahidi kushirikiana nae katika kuhakikisha kuwa wanaleta magauzi na kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari jijini dsm Mwekiti mwenza wa Umoja huo James Mbatia amesema Umoja huo umetafakari na kutoa fursa kwa kila mtanzania mwenye kutaka mageuzi ajiunge na umoja huo ili waunganishe nguvu ya kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani.

Kutokana na Tamko hilo waandishi wa habari waliokuwapo katika mkutano huo walitaka ufafanuzi Juu ya kumkaribisha Bwana Lowasa huku viongozi hao awali walikuwa wakimshutumu kuhusika na Ufisadi katika sakata la Richmond na kusababisha kujiuzuru kwake.

M/kiti mwenza wa Ukawa Prof.Ibrahim Lipumba amesema Tatizo la Ufisadi alilotuhumiwa Bw.Lowasa linatokana na Mfumo uliopo katika Chama cha mapinduzi na Serikalini .

Aidha Waandshi wa habari pia walitaka kujua kuhusu nafasi ya Ugombea Urais Kupitia umoja huo ikiwa Lowasa atakubali kujiunga nao Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa  Emmanuel  Makaidi anaeleza...

Hata hivyo Prof.Lipumba amesema Suala na Mgombea Urais kuchelewa kutangazwa linatokana na marekebisho na makubaliano ndani ya vyama husika na Umoja huo lakini akaweka wazi kuwa mgombea urais kupitia Umoja huo atatangazwa kabla ya tarehe moja mwezi  agosti .


Mwekiti mwenza wa Umoja huo James Mbatia akitoa tamko hilo,la kumkaribisha Lowasa mbele ya waandishi wa habari jijini dsm

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube