BREAKING

Monday, 20 July 2015

THE STARS BAND YAZINDULIWA RASMI SIKU YA EID MOSI NDANI YA MZALENDO PUB HUKU IKISINDIKIZWA NA BENDI YA FM ACADEMIA PAMOJA NA BARNABA

Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Aneth Kushaba imezinduliwa rasmi siku Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikisindikizwa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.  

Mkurugenzi wa The Stars Band, Aneth Kushaba akijitambulisha kwa mashabiki wakenm  pamoja na azungumza na wapenzi wa bendi mpya ya The Stars Band wakati wa uzinduzi yeye binafsi alisema hawezi kusema yaliyopita bali wapenzi wa bendi hiyo wategemee makubwa kutoka kwenye bendi hiyo iliyozinduliwa siku ya Idd Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano akionesha mambo yake kwenye stage hii yote ni wakati anajitambulisha kwa mashabiki wa bendi waliofika kwenye uzinduzi wa bandi hiyo

Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Seghito mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangozi akijitambulisha kwa kuonesha uwezo wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika katika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar
Mpiga Drums na pia ndiye meneja wa Bendi, Kibosho akijitambulisha kwa kuone uwezo wake katika Drums
 Mpiga la Gitaa katika Bendi ya The Stars, Othuman Majuto akionesha ujuzi wake kwenye stage wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
   Mpiga la Gitaa la Base katika Bendi ya The Stars, Zaid Sato (Base) akionesha mambo yake kwenye stage
  Mpiga la Keyboard katika Bendi ya The Stars,  Sebastian akionesha maujaja yake
  Mpiga la Keyboard katika Bendi ya The Stars, Denis akifanya ya kwake
 Mwimbaji wa Bendi ya The Stars,  Alawy Junior akijitambulisha rasmi wakati wa Uzinduzi wa Bendi hiyo Mpya iliyojaa vipaji vya ukweli
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Prince ambaye aliwavutia walembo wengi kutokana na sauti yake wakati wa kujitambulisha wakati wa uzinduzi wa Bendi hiyo.
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Mao Santiago akijitambulisha kwa kuimba sebene moja matata ilikuwa ni hatari
Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba moja ya nyimbo zake huku akisindikizwa na waimbaji wa Bendi ya The Stars kutshoto ni Seghito na kulia ni Prince

Mwimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiendelea kutoa burudani ndani ya kiota cha Mzalendo Pub wakati wa Uzinduzi wa Bendi mpya ya The Stars iliyozinduliwa siku ya Idd - Mosi
wimbaji wa Bongo Flava, Barnaba Elias aka Barnaba akiimba sambamba na  Mwimbaji wa Bendi ya The Stars,  Alawy Junior wakati wa uzinduzi wa sendi mpya ya The Stars 
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakiimba kwa pamoja wakati wa Uzinduzi wa Bendi hiyo ndani ya Kiota cha Mzalendo Pub, KIjitonyama jijini Dar
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Seghito  (wa pili kutoka kushoto) akiimba moja ya nyimbo zinazobaba katika dunia hii huku akisindikizwa na waimbaji wenzake amabo ni Felly Kano(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Bendi, Aneth Kushaba( wa pili kutoka kulia) pamoja na Prince (wa kwanza kulia)
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' ambao ni  Jesus(wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Patcho Mwamba(wa pili kutoka kushoto),  Pablo Masai (katikati), Mulemule(wa pili kutoka kulia) pamoja na 33 wote wakiimba kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa bendi mpya ya The Stars katika kiota cha Mzalendo Pub 
RAIS wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', Nyoshi El Sadat akiimba kwa hisia kali wakati wa uzinduzi wa bendi ya The Stars iliyofanyika kwenye kiota cha Mzalendo Pub siku ya Idd-Mosi
Wakati wa uzinduzi wa Bendi ya The Stars ilikuwa ni funika mbayaaaaa maana  Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma ilifanya ya kwao
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa na Totoo Kalala(wa kwanza kusoto) pamoja na MP 3 (wa kwanza kuli) wakiendelea kutoa burudani huku wakisindikizwa na waimbaji pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo
Ni burudani kwenda mbele
Wanenguaji wa bendi ya  Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiendelea kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa bendi mya ya The Stars
Waimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadat wakiendelea kutoa burudani wa wapenzi wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma pamoja naThe Stars Bandi
Mwimbaji wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wakiongozwa, Totoo Kalala(wa kwanza kusoto) akiendelea kuimba huku akisindikizwa na wanenguaji wa bendi hiyo
Burudani ikiendelea 
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakendelea kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd Mosi katika kiota cha Mzalendo pub
Wakiendelea kucheza kwa furaha wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano(wa pili kutoka kulia) akiimba kwa hisia kali huku akisindikizwa na na waimbaji wenzake ambao ni Mao Santiago(wa kwanza kushoto), Seghito (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba
Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) akiimba na Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Felly Kano ambao kwa pamoja wameamua kuitumia fursa walioipata kupitia vipaji vyao vya kuimba.
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd Mosi atika kiota cha Mzalendo Pub jijini Dar
Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) akiimba na Mwimbaji mwenzake wa Bendi ya The Stars, Seghito wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars, Mao Santiago( wa pili kutoka kushoto) akiendelea kuimba sebene za nguu uku akisindikizwa na waimbaji wenzake ambao ni Seghito(wa kwanza kushoto), Felly Kano (wa pili kutoka kulia) pamoja na Alawy Junior(wa kwanza kulia)
Ndani ya Bendi mpya ya The Stars ni full burudani na sio chenga
The Stars Band wakiendelea kutoa burudani
Mwimbaji wa Bendi ya The Stars,  Alawy Junior(kushoto) akiimba sambamba na Mkurugenzi wa Bendi ya The Stars, Aneth Kushaba(kushoto) wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika siku ya Idd-Mosi katika kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar
Ndani ya bendi ya The Stars ni full raha hapa waimbaji wa bendi hiyo wakionesha moja ya style yao kwa mashabiki waliofika kwenye uzinduzi huo
Mashabiki wa Bendi ya The Stars wakiendelea kuserebuka na ngoma za bendi hiyo wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Waimbaji wa Bendi ya The Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo
Wazee wa kusababisha hara za mziku zinakua poa kutoka katika bendi ya The Stars wakiwa kwenye picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube