Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, akithibitisha taarifa iliyokuwa ikizagaa mitandaoni ya Wagombea Urais walioingia katika hatua ya tano bora, ambao aliwataja kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali. Majina hayo yanapelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kujadiliwa na kupatikana matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndie atakuwa Mgombea Urais.
CHANZO: MTAA KWA MTAA BLOG
CHANZO: MTAA KWA MTAA BLOG
No comments:
Post a Comment