Kuna taarifa za kuwa mshambuliaji wa Singida United, Mnyarwanda, Danny Usengimana ameondoka ndani ya kikosi chake baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kummalizia fedha zake za usajili na kuamua kurejea kwao,
Rwanda.
Chanzo cha habari kimedai kuwa Usengimana aliondoka ndani ya timu hivi karibuni baada ya kushindwa kuelewana katika maslahi na inadaiwa anaidai timu hiyo kiasi cha fedha zake za usajili ambazo hajamaliziwa na si yeye
pekee bali kuna wachezaji wengine ambao wanadai fedha hizo.
Hata chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kudai kuwa mchezaji huyo imebidi kuondoka kambini na kuweza kurejea nchini kwao Rwanda huku timu ikiwa kambini kwa maandalizi ya FA dhidi ya Yanga.
Alipotafuywa Mkurugezni wa Singida United, Fest Sanga kuweza kupata taarifa kuhusiana na mshambuliaji huyo:
“Kwa sasa timu ipo inaendelea na maandalizi hapa kambini na Danny Usengimana ni kweli hayupo amerejea kwao kwa ruhusa maalum baada ya kuwa na matatizo ya kifamilia
akimaliza ataungana na wenzake inaweza kuwa kabla ya mchezo na Yanga au baada ya mchezo huo.”
No comments:
Post a Comment