Wednesday, 30 June 2021
ENGLAND WANA JAMBO LAO EURO 2020....WAICHAPA UJERUMAN 2-0
EURO 2020- UKRAINE HIYOOO ! ROBO FAINALI
Michuano ya EURO 2020 imeendelea kutikisa katika hatua ya robo fainali ambapo katika mchezo wa hatua ya 16 bora Ukraine imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sweden.
Nyota wa mchezo huo Oleksandr Zinchenko alifunga bao dakika ya 27 bao ambalo baadae ililisawazishwa na mchezaji Emil Forsberg.
Dakika 90 za mchezo wa kawaida ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Baadae ziliongezwa dakika 30 na nyota Artem Dovbyk alipachika bao dk 120 na kuifanya timu yake ya Taifa ya Ukraine kutinga hatua ya robo fainali.
Timu ya Sweden ilipata pigo baada ya mchezaji wao Marcus Danielson katika dakika ya 99 alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya Sweden kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu.
Tuesday, 29 June 2021
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCMA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KAMATI KUU YA TAIFA -DODOMA
WAZIRI MKENDA AIPA RUNGU BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA KAHAWA
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizindua Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa yenye makao makuu Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Juni 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa ambayo ipo chini ya wizara ya kilimo kujiimarisha kiutendaji kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa.
Waziri Mkenda ametoa maelekezo hayo tarehe 29 Juni 2021 wakati akizindua Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Kahawa Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Waziri Mkenda ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha kuwa inaongoza sekta hiyo kwa kuwa na mawazo ya kibiashara ili kuwanufaisha wakulima na kuinufaisha nchi.
“Ninyi nyote mlioteuliwa wasifu wenu ndio muelekeo wetu, mnapaswa kufanya maamuzi mazuri kwani tunachotaka ni wakulima wetu kupata pesa za kukidhi mahitaji yao, mkifanya maamuzi ya kumuumiza mkulima yatakuwa hayatusaidiii” Amekaririwa Waziri Mkenda
Kadhalika Waziri Mkenda ameitaka Bodi hiyo kutathmini wingi wa minada ya kahawa ambayo imegawanywa kwenye kanda kama ina tija kwa maendeleo ya zao la kahawa nchini.
“Mimi sijaja kuwashauri ninyi kwa kuwa ninyi ndio mmeteuliwa pia kwa ajili ya kunishauri mimi lakini hili la minada tazameni muone kama lina akisi matakwa ya biashara ya kahawa” Amekaririwa Prof Mkenda
“Pia hakikisheni tunaimarisha uzalishaji na tija kwenye kahawa ili tuweze kuuza kwa bei nzuri na kuwashinda wengine, kwani namna pekee ya kushindana kwenye bei ni kuongeza tija”
Wajumbe walioteuliwa kuunda Bodi ya Kahawa inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Aurelia K. N. Kamuzora, ni Enock Chimagu Nyasebwa, Edson M. Rugaimukamu, Shadrack A. Issangya, Gotham Filipo Haule, Tinson Nzunda, Neel Vohora, Nangula H. Mwampamba, na Bahati Ludhabiho Mlwilo.
Mhe.RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN ATUA JIJINI DODOM AKITOKEA DAR ES SALAAM.
RC SENDIGA APIGA MARUFUKU WANANCHI WA IRINGA KUTUPA TAKA HOVYO UKIKUTWA FAINI 50,000
Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga amepiga marufuku wananchi wote kutupa takataka na kuchafua mazingira hovyo ili kuendelea kuyaweka mazingira kuwa masafi na na kuepuka kukumbana na magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo,mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alisema kuwa mkoa wa huo umekuwa na sifa ya kuwa mkoa ambao unafanya vizuri kwenye swala la usafi hivyo wanapaswa kuendelea kufanya usafi na kuyaweka mazingira safi.
Alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa wanatakiwa kuzingatia kutotupa takataka hovyo kuanzia kwenye magari,nyumbani na kwa wananchi wanaotembea kwa miguu ili kuuweka mji safi na kuwa mkoa wenye mazingira bora.
Sendiga alisema kuwa kuna changamoto za wananchi kutupa takataka kwenye mifereji ya maji machafu na kuzitelekeza taka hizo ambazo zimekuwa zikichafua mazingira hivyo wananchi wanatakiwa kusafisha mifereji yote kwa wakati ili kuokoa kusitokee mafuriko kipindi vua zikianza kunyesha.
Alisema kuwa licha ya mazingira ya mkoa wa Iringa kuendelea kuwa masafi lakini bado kuna changamoto kubwa kwa kuwa na baadhi ya maeneo hayaridhishi kama maeneo mengi hivyo juhudi binafsi za viongozi zinatakiwa kuhakikisha mitaa hiyo usafi unafanyika.
Sendiga alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kuwa mkoa wa Iringa unashika namba moja kwa kuwa na mazingira bora na masafi na kuongoza kwa usafi kitaifa kama ambavyo ilikuwa miaka ya nyuma.
Kwa upande wake afisa mazingira wa manispaa ya Iringa Abdon Mapunda alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu ya usafi kwa wananchi wote ili wajue umhimu wa kutunza mazingira yanayowazunguka.
Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kulipa ada ya taka ili kuviwezesha vikundi vya usafi kuendelea kufanya usafi na kutunza mazingira vizuri ya halmashauri ya manispaa ya Iringa.
Mapunda alisema kuwa mwananchi akikamatwa ametupa takataka hovyo na kuchafua mazingira atatozwa faini ya shilingi elfu hamsini (50,000) huku lengo lake likiwa kuhakikisha wananchi wanajifunza namna bora ya utunzaji wa mazingira.
Mapunda alisema kuwa wananchi wa manispaa ya Iringa wanatakiwa kuendelea kufanya usafi na kuyatunza mazingira kwa lengo la kuendelea kulinda afya kwa kuishi katika mazingira masafi.
Alimalizia kwa kusema kuwa wamezindua kampeni ya Iringa safi lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya kuharibika kwa magari ya kubebea taka mara kwa mara jambo linalosababisha kupunguza kasi ya uzoaji wa taka.
Naye mratibu wa kampeni ya Iringa safi Paulo Myovela alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wananchi wa manispaa ya Iringa wanafanya usafi na kuyapenda mazingira yao.
Alisema kuwa kampeni hiyo inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa vifaa vya kukusanyia taka taka katika halmashauri hiyo hivyo viongozi na wadau mbalimbali kuhakikisha wanachangia jinsi ya kupatikana kwa vifaa hivyo.