BREAKING

Monday, 23 April 2018

DOGO MUINGEREZA JADON SANCHO,MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI AFUNGA BAO LIGI YA UJERUMAN



DORTMUND, Ujerumani

Mshambuliaji  Jadon Sancho ameweka rekodi ya kuwa Muingereza mwenye umri mdogo zaidi kufunga bao katika Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’.

Jadon aliweka rekodi hiyo juzi wakati alipoifungia timu yake ya Borussia Dortmund bao kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bayer Leverkusen. Ligi hiyo, hapa Bongo unaitazama kwa bei nafuu sana kupitia King’amuzi cha StarTimes.

Sancho alitupia bao hilo katika dakika ya 13 kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park, kutokana na mpira wa kona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 pia alitengeneza asisti mbili kwa Maximilian Philipp na Marco Reus katika kipindi cha pili na hivyo kumfanya kuwa na siku nzuri.



Akizungumza mara baada ya mchezo huo, chipukizi huyo anasema: "Nilipata nafasi mara ya kwanza sikuitumia vizuri, ilinisikitisha kwa kuwa muda huyo matokeo yalikuwa 0-0.

"Nilipopata nafasi nyingine nikaitumia vizuri, nina furaha nimefunga bao langu la kwanza nikiwa hapa. 

"Limekuwa jambo gumu kurejea kwenye kikosi, kuwa fiti na sasa ninajisikia vizuri."


Sancho amekuwa Muingereza wa pili kufunga bao msimu huu katika Bundesliga, mwingine alikuwa ni Ademola Lookman wa RB Leipzig.

Chipukizi huyo alijiunga na Dortmund mwanzoni mwa msimu huu akitokea Manchester City, alicheza mchezo huo ukiwa ni wa tisa kwake na wa nne kuanza katika kikosi cha kwanza.




Neuer arejea uwanjani, kocha afunguka

MUNICH, Ujerumani

KOCHA Mkuu wa Bayern Munich, Jupp Heynckes amezungumzia juu ya kipa wake, Manuel Neuer ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita sasa kuwa ana mpango wa kumtumia kabla ya msimu huu haujafikia tamati.

Neuer, alikuwa majeruhi tangu alipoumia mguu katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mainz katika mechi ya Septemba 16, 2017, ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza tangu Ijumaa iliyopita.

"Tunafurahia jinsi anavyoendelea,” alisema Heynckes na kuendelea: 




"Tunafanya kila kitu kiwe sawa kwa sasa lakini ni mapema sana kuzungumzia kuhusu lini atarejea uwanjani, najua ninachokifanya, nina mpango naye muhimu.”

Bayern bado inasubiri kucheza fainali ya DFB Cup, pia ina mechi za Ligi ya Mabingwa pamoja na mechi chache za Bundesliga licha ya kuwa wameshatwaa ubingwa.

Kabla ya kuumia, Neuer alikuwa mmoja wa makipa bora duniani, kurejea kwake kunaweza kuwapa nguvu Ujerumani kuelekea katika michuano ya Kombe la Dunia ambayo pia itarushwa na StarTimes.






WATAKA SHERIA YA WATIA MIMBA WANAFUNZI IONGEZWE MENO


Wito umetolewa kwa serikali kuhakikisha wanawadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika wamebaka au kuwapa mimba wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari nchini.

Baadhi ya wadau wa Elimu Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano huo.
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wa elimu wilaya ya mvomero mkoani Morogoro wakati wa mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania TEN /MET ili kupeana mrejesho wa namna ya kukabiliana na changamoto za mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.


Katika mkutano huo wa wadau  wamebaini ushiriki wa karibu wa wazazi na watoto wao haupo kwa kiasi kikubwa jambo linaloelekea kuendelea kuwepo kwa changamoto hiyo.


Kwa upande wake afisa elimu wa wilaya hiyo Bi. Maajabu Nkamyemka amesema kwa wilaya ya mvomero takwimu zinaonesha hadi April 6 mwaka huu takribani mimba 90 zimebainika kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo miongoni mwa hizo mimba 13 ni kutoka shule za msingi.

Aidha Bi. Nkamyemka amesema kuwa ni jukumu la wazazi na walimu kwa kushirikiana na wanafunzi kuhakikisha wanawafichua wale wote ambao ni wahusika bila kuwafumbia macho ili sekta husika kupambana nao ili kutokomeza janga hilo.

"kwa kuwa binti akipewa ujauzito huwa tunahangaika tu na aliyempa ujauzito, na yule mwenye ujauzito tunamuacha sasa bhas sasa kwa kuwa wazazi hawataki kuleta ushirikiano tutamfungulia kesi mwanafunzi mwenye mimba pamoja na wazazi ili wazaz wawachunge watoto wao ipasavyo "Alisema Nkamyemka.
Wadau hao wa elimu wakiwa ndani ya mkutano huo 
Naye mratibu elimu wa kata za mhonda na Kweuma bwn, Heriamini Mariki amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya mimba hasa kwa wanafunzi, wa sekondari jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wazazi ndiyo chanzo cha tatizo hilo huku akitaja sababu zinazochangia kuwa ni pamoja na uelewa finyu wa wazazi na wakati mwingine umaskini kwa baadhi ya kaya nyingi wilayani humo.

 “Sisi kama wadau wajibu wetu mkubwa ni kuwapatia elimu wazazi juu ya athari za kutokaa karibu na watoto wao na kuwa wawazi juu ya madhara ya kufanya ngono wakiwa na umri mdogo" alisema Mariki

Naye diwani wa kata ya mhonda Bw. Abdallah Hassani Khalifa ametoa rai kwa Serikali kujenga hosteli kwa shule za kata ili kuondokana na tatizo la mimba za utotoni linaloikumba nchi nzima kwa kiasi kikubwa, huku akiwataka wazazi na walimu wanawapa  watoto wanafunzi ushirikiano wa kutosha na ulinzi kwani ndiyo haki pekee wanaotakiwa kuzipata ili kufanya vyema katika masomo yao.


WANANCHI WA KIJIJI CHA LUMWAGO MAFINGA MJINI WASHANGILIA KUWAKA KWA UMEME TOKA WAMEZALIWA

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam,Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi pamoja na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi wakiwa nafungua na kuwasha umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji cha Lumwago kata ya Upendo Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani Iringa.

Friday, 20 April 2018

HIVI NDIVYO YANGA WALIVYOTUA USIKU WAKITOKEA ETHIOPIA


Kikosi cha Yanga kimewasili usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam kikitokea Ethiopia majira ya saa 7 na kupokelewa na baadhi ya mashabiki hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JK Nyerere.

Yanga ilisafiri kwenda Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Africa dhidi ya Wolaita Dicha SC.

Thursday, 19 April 2018

DSTV KUWALETEA FIFA WORLD CUP CHANNEL MAALUM


Wapenzi na wateja wa DStv, ni nafasi yenu sasa ya kufurahia msimu wa Kombe la Dunia kwani tumekuletea chaneli maalum itakayokuwa ikirusha matukio  matukio yote muhimu yaliyojiri kwenye historia ya Kombe la Dunia kuanzia ilipoanza mpaka sasa! Chaneli hii inapatikana sasa  kwa wateja wote wanaotumia  king’amuzi cha DStv, Supersport 214 iliyopo kuanzia kifurushi Bomba.

Wewe mpenzi wa soka ambae unalisubiri kwa hamu FIFA Kombe la Dunia 2018, Angalia sasa chaneli hii maalum yenye matukio maalum ya Kombe la Dunia,  kupitia chaneli hii Supersport 214 utakuatana na 
  • Historia ya mashindano ya Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1966 mpaka 2012
  • Mechi zilizotamba na kufanya vizuri ndani ya Kombe la Dunia
  • Mahojioano mbalimbali pamoja na wachezaji
  • Makala za Lombe la Dunia

Kubwa kuliko ni kwamba  chaneli hii maalum iliyoanza rasmi tarehe 18 Aprili na itaendelea kuwepo mpaka tarehe 12 Juni inapatikana kwenye king’amuzi cha DStv pekee, kuanzia kifurushi Bomba kwa sh.19,000 tu, chaneli namba 214.
Pata Ladha na burudani ya Kombe la Dunia kabla ya Kombe la Dunia  2018 kuanza kupitia ndani ya DStv pekee!


Wednesday, 18 April 2018

WAKULIMA MKOANI IRINGA WATAKIWA KUTUMIA MBOLEA YA YARA INAYOZALISHWA NA KAMPUNI YA YARA TANZANIA

Afisa Masoko wa Kampuni ya Mbolea ya Yara mkoa wa Iringa Dionis Tshonde akitoa maelezo kwa kiasi gani mbolea hiyo inawasaidia wakulima kulima kilimo chenye tija na kuvuna mavuno mengi kwenye msimu mmoja 
 Uongozi wa timu ya Singida United ya mkoani Singida na wachezaji wa timu hiyo nao walifanikiwa kutembelea shamba darasa ambalo wanatumia mbolea ya kampuni ya Yara na kuwataka wakulima wa mkoani Iringa kulima kilimo bora kwa kutumia mbolea ambazo zinazalishwa na kampuni ya Yara iliyopo kulasini jijini Dar es salaam.
Shamba darasa ambalo lipo mkoani Iringa katika kata ya Ruaha manispaa ya Iringa

Wakulima wametakiwa  kutumia  kulima kilimo chenye tija kwa kufuata maelekezo ya wataalamu  ili waweze kupata mazao bora.
Hayo yamesemwa na Afisa Kilimo Manispaa ya Iringa Bi.Happines Nnko wakati akizungumza na wakulima wa kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa katika shamba darasa ambalo wakulima wamelima kwa kufuata kanuni na taratibu za kilimo bora na kufanikiwa kustawisha mazao vizuri.

Hapinpines alisema kuwa wakulima wanapoteza nguvu,muda kulima kilimo sikichokuwa na tija kwa kutofuata  kanuni za kilimo, mbegu bora na mborea za kupandia na kukuzia.

"Ninawaomba tuwatumie wataalamu wetu ili tuweze kulima kilimo chenye tija.Pia ninawaomba haya mliyoshauriwa na wataalamu kutoka kmpuni ya Mbolea Yara na Seed.co mkayafanyie kazi,lengo tunataka kuona kilimo kikimkwamua Mkulima na si kumdidimiza"

Akitoa Elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa kutumia Mbolea ya Yara  Vespa Kwavava,amabae ni Mkulima katika eneo la Ipogolo kata ya Ruaha alisema kuwa hapo awali  kabla hajaanza kutrumia Mbolea uzalishaji  ulikuwa mdogo ,lakini kwa hivi sasa umeongezeka.

Ninawaomba wakulima wenzangu watumie mbolea na wataalamu ili wawaeze kupiga hatua katika uzalishaji na hatimae kujikwamua kimaisha kupitia kilimo.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Dionis Tshonde alisema kuwa wataendelea kutoa elimu ya kilimo bora kwa kushirikiana na wananachi ili kuhakikisha wanalima kilimo chenye faida kubwa kuliko wanavyofanya sasa wakulima wengi.

“Wananchi wengi wanapenda kulima lakini bado hawafuati taratibu na kanuni za kilimo bora hivyo atahakikisha kupitia kampuni ya Yara wanatoa elimu kwa wakulima ili kuwakomboa katika kilimo wanacholima kwa sasa hadi kufikia kulima kilimo cha kisasa na chenye faida” alisema
  
Tshonde aliwataka wakulima kutumia mbolea za kampuni ya Yara ambazo kwa sasa ndio imekuwa mkombozi wa wakulima kwa kuzalisha mazao mengi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Mbolea za kampuni ya Yara zinavirubisho ambavyo vinasaidia mazoa kukuwa na kuzalisha mazao mengi ambayo yanakuwa faida kwa wakulima”

Tshonde alisema kuwa ukitumia mbolea ya kampuni Yara utapata faida kubwa kwa kuwa ukilima hekali moja unakuwa na uhakika wa kuvuna kati ya gunia 35 hadi 40 endapo mkulima atazingatia kanuni na taratibu za kilimo che tija.

Monday, 16 April 2018

MULTICHOICE YAZIDI KUWAFIKIA WATEJA WAKE YAZINDUA KITUO CHA HUDUMA MWANZA

 Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo maalum cha huduma jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Kanda John Kasuku


Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akitoa maelezo kuhusu kituo maalum cha huduma jijini Mwanza mara tu ya ufunguzi wa kituo hicho mwishoni mwa wiki. 

Katika kuhakikisha kuwa inaimarisha na kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja, kampuni ya MultiChoice Tanzania imefungua kitua kipya cha huduma  jijini Mwanza.

Kituo hicho kilichofunguliwa mwishoni mwa wiki ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo kuwasogezea wateja wake huduma karibu ambambo hivi karibuni, kituo kama hicho kilifunguliwa mlimani City jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo amesema kituo hicho ni cha Kisasa na kinaweza kuwapa wateja wa DStv huduma zote kuanzia kununua vifaa, kufanya malipo, ufundi na huduma kwa wateja.

Amesema huu ni mkakati maalum wa MultiChoice Tanzania kufungua vituo kama hivyo kote nchini ambapo hivi karibuni  vituo zaidi vitafunguliwa katika miji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Dodoma.

Hivi sasa mkakati wetu mkubwa ni kuhakikisha kuwa mteja aliyeko mkoani anapata huduma sawasawa na yule aliyepo Dar es Salaam kwani vituo hivi vya huduma vimeboreshwa na kuwa na uwezo wa kutoa kila aina ya huduma alisema Shelukindo.

Amewataka wateja wa DStv jijini Mwanza kukitumia kituo hicho kwa ufanisi na pia sasa kampuni hiyo pia inaimarisha timu yake ya mauzo, kuongeza idadi ya mawakala ili kuhakikisha kuwa wateja wanahudumiwa kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.

Kuhusu changamoto za kiufundi, Shelukindo amesema hili sasa limepatiwa ufumbuzi kwani MultiChoice imetoa mafunzo maalum ya ufundi kwa mamia ya vijana kote nchini kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake. Amesema kuanzia sasa kutakuwa na mafundi maalum walioidhinishwa ambao wamepatiwa mafunzo maalum.  

Sunday, 15 April 2018

MATUKIO MBALIMBALI YA NAIBU WAZIRI WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII JAPHETI NGAILONGA HASUNGA AFANYA ZIARA KATIKA PORI LA KONDOA DODOMA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata alipokuwa akitoa maelekezo kwa Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la la akiba la Mkungunero alipofanya ziara katika pori hilo jana Wilayani Kondoa
Maafisa hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo ya namna bora ya usimamizi wa hifadhi za wanyamapori alipofanya ziara katika pori hilo jana Wilayani Kondoa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa kikao na  Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa. Wakwanza kulia kwake ni Meneja wa pori la akiba la Mkungunero Bw. Emmanuel M. Birasso na Meneja wa pori la akiba la Swaga Swaga Bw. Alfred Choya.

: Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (katikati) akimsikiliza Diwani wa Kata ya Bumbuta Bw. Bashiru Mtoro (kulia) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kulia) akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa Bi. Hija Suru (kushoto) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana. Kulia kwake  ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (katikati) akitizama sehemu ya ng’ombe waliokamatwa na Maafisa wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero kwa kuingia katika hifadhi hiyo wakati  alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori la Mkungunero jana Wilayani Kondoa, ambapo zaidi ya ng’ombe 250 wanashikiliwa. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi – Usimamiziwa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata na kulia kwake ni Kaimu Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kondoa Bw. Juma Solomon Nyamwakirya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akitoa maelekezo kwa  Kaimu Mkurugenzi  – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata wakati wa kikao na  Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafugaji wa vijiji vinavyozunguka pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akimsikiliza Bw. Yohana Bilo ambaye ng’ombe wake wanashikiliwa na Maafisa Hifadhi wa pori la Mkungunero kwa kuingia katika pori hilo alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube