BREAKING

Wednesday, 31 May 2017

MULTICHOICE TANZANIA WAWAJAZA ZAWADI WADAU WAO KATIKA SIKU MAALUM YA KIAFRIKA

 Wadau wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kuhudhuria siku maalum ya Kiafrika iliyoandaliwa na Multichoice Tanzania kushoto ni John Bukuku, ambaye ni Mkurugenzi wa Fullshangwe, kulia ni Mkurugenzi wa mtandao wa Shamakala360, Said Makala
 Mwakilishi wa Multichoice Tanzania  Esther akimkabidhi zawadi maalum Mdau wa Mtandao wa LIMUTUZ William Cheyo, ikiwa ni maalum katika siku ya Kiafrika.
 Mwakilishi wa Multichoice Tanzania  Esther akimkabidhi Mdau wa Mtandao wa Shamakala360 zawadi maalum ya kuadhimisha siku ya kiafrika, Said Makala, ambaye pia ni Mtangazaji Channel Ten.

TBS YAWASHAURI WAZALISHAJI WADOGO WADOGO WA BIDHAA KUTUMIA FURSA YA BURE YA UKAGUZI

Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes Kaseka pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga .

Alisema kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.

"Bado wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na sasa" alisema Kaseka.

Aidha alisema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanaziondosha katika soko bidhaa ambazo ni hafifu kwa kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara katika masoko na maeneo yote yanayohusika na shughuli za uuzaji wa bidhaa.

Nae Mfanyabiashara Aisha Kisoki alisema kuwa changamoto kubwa ni muingiliano wa bidhaa kutoka nje ambazo kwa hapa nchini zinauzwa kwa bei rahisi tofauti na wanazozizalisha.

Alisema kuwa iwapo TBS wataweza kudhibiti uingiaji usio rasmi wa bidhaa kutoka nje utasaidia sana wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuona umuhimu wa kuweka nembo bidhaa zao.

Tuesday, 30 May 2017

MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI TANGA


Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa wakazi wa Jiji la Tanga kwenye banda lao lililopo katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara ya kimataifa
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiptia kwenye banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) wakati alipofungua maonyesho ya kimataifa ya  biashara ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akisalimiana na mmoja wa watumishi Tanapa wakati wakati alipotembelea banda lao kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiendelea na shughuli ya kukagua mabanda ya Maonyesho
Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
 Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao
 Afisa Habari za Utalii (TTB William Akile kulia akiongeza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda lao

 Maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga katika Banda lao lililopo kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunapofanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tano kutoka kushoto ni Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo katikati ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu na kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens
 kulia ni Sabrina Komba ambaye ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kulia ni Afisa matekelezo Macrina Clemens wakimsikiliza kwa umakini mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alifika kwenye banda lao kupata ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na mfuko huo
 Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens kulia akisitiza jambo kwa mkazi wa Jiji la Tanga kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali muhimu ikiwemo za matibabu kushoto ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Mwakababu katikati ni  Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kulia kwake ni Afisa Masoko na Elimu kwa umma makao makuu Sabrina Komba

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa tayari kutoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Tanga kuhusu namna wanavyoweza kunufaika kupitia mfuko huo
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga ambaye alitembelea banda lao
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kuhusu faida za wakazi wa Jiji la Tanga kujiunga na mfuko huo lakini pia namna walivyojiandaa na ujio wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MULTICHOICE TANZANIA YASHEREKEA SIKU YA AFRIKA




Kwa kipindi kizima cha mwezi wa 5 (Mei) wateja wa DStv wamekuwa wakifurahia zaidi vipindi  vyenye ubora na vya kusisimua  vya Kiafrika.
Huba, Jikoni na Marion, Mchikicho wa Pwani, Yahusu Tanzania, Kimbembe ni kati ya vipindi kutoka Tanzania vilivyo bamba mwezi huu ndani ya chaneli Maisha Magic Bongo (DStv 160)
Meneja Mahusiano Multichoice Tanzania, Johnson Mshana amesema, “Mwezi Mei kwetu tumeufanya kuwa mwezi maalum kwa ajili ya kutangaza na kujivunia  utajiri wetu  waafrika ikiwa ni pamoja na utamaduni na Sanaa na michezo
Hii ni moja ya sehemu ya ahadi ya  DStv kwa kutoa ushirikiano kwenye  sekta ya sanaa na burudani kwa kuendelea kusaidia Filamu za Afrika na kwa kuwekeza katika watu, mawazo na vipaji.
Ikiwa ni njia moja wapo ya kusheherekea mwezi huu wa Afrka, Wafanyakazi  wa Multichoice Tanzania waliamua kuvaa mavazi maalum ya Kiafrika na kuandaa chakula maalum cha kiafrika kwa wafanyakazi wote.
Haikuishia hapo, Multichoice Tanzania pia imeandaa zawadi maalum za Kiafrika kwa waandishi wa habari, ikiwa ni njia ya kuonyesha shukrani kwa waandishi na kudumisha Umoja na Uafrika wetu.
#AFRIKAYETU

Monday, 29 May 2017

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KOREA KUSINI, AHOJIWA NA CCTV YA CHINA, LEO

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini hapa nchini, Song Geum-Young  alipomkaribisha katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam, leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini hapa nchini, Song Geum-Young Katika mazungumzo yao, Katika mazungumzaa hayo, wamehimiza suala la kuboresha mahusiano baina ya Jamhuri ya Korea Kusini na Tanzania pamoja na kuzungumzia ushirikiano wa muda mrefu katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akihojiwa na Mwanishi wa Kituo cha Televisheni cha China Central Television - CCTV kuhusu mafanikio ya kiuchumi ambayo China imeyafikia na hatua mbalimbali za maendeleo ambazo Tanzania inajifunza na kushirikiana na China ili kufanikiwa kufikia uchumi wa kati.

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA WAIVA



 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia akimueleza jambo  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kushoto wakati alipofungua maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
 Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale akizungumza na waandishi wa habari leo


MRADI wa Bomba la Mafuta Mkoani Tanga umefikia kwenye hatua ya wataalamu kukagua njia itakayopitisha miundombinu ya bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.


Hatua hiyo imekuja baada ya serikali ya Tanzania na Uganda kutiliana saini ya mkataba baina ya nchi na nchi (Iga) kukamilika.


Hayo yalisemwa leo na Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.


Alisema tayari wameshafanya maamuzi yameshakamilika wataalamu wanafanya tathimi ya udongo katika njia ambayo bomba hilo litapita kwa taarifa ya awali njia iliyopatikana upana mita 200 na baadae watalaamu wataipunguza mpaka 100.


Awali akizungumza kuhusiana na mradi huo, Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Augustino Kasale alisema mradi huo utapita katika mikoa nane ya Tanzania na kuzalisha ajira 10000 za kudumu na muda mfupi.


Alizitaja fursa ambazo zitakuwa moja kwa moja ni hutoaji huduma wakati wa ujenzi, ajira za muda mfupi na moja kwa moja, fursa za usafirishaji ikiwemo kuufungua mkoa wa Tanga kiuchumi.


“Hivyo hivi sasa wananchi wa mkoa wa Tanga wanapaswa kujiandaa na ujio wa Bomba la Mafura ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi Mkoani Tanga “Alisema.


MD KAYOMBO ASHAURI WATANZANIA KUFUATA FURSA ZILIPO

Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuzifuata fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kukuza uchumi wa viwanda.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza wakati akitoa taarifa ya mbio za Mwenge unaotaraji kuzuru katika Manispaa ya Ubungo Tarehe 31, Mei 2017.

Alisema kuwa katika mikoa mbalimbali Mwenge wa Uhuru ulipopita umekutana na fursa ambazo Watanzania wakizitafuta na kuzifanyia kazi wataondokana na uvivu, kukaa bila kufanya kazi na umasikini kwa kuwa sasa Serikali iliyopo madarakani ni ya kazi.

Aliongeza kuwa, nchi nyingi zimekuwa kiuchumi kupitia viwanda na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda, wananchi wanapaswa kuzichangamkia fursa mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya Serikali kufikia uchumi wa viwanda.

MD amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Ubungo utapita katika Miradi mitano ya Maendeleo ambapo Miradi minne kati ya hiyo itazinduliwa na Mradi mmoja wa Ujenzo wa Kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la Msingi.

Alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu jumla ya shilingi Bilioni 2,854,647,991.89

Imetolewa Na;
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO

Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasalimu wanamichezo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Baadhi ya wanamichezo kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam wakifatilia mchezo kati ya Ilala na Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na mchezaji wa Mpira wa Miguu Manispaa  ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto), Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno (Katikati) na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Khamisi Lissu wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa hamasa kwa timu ya UMISSETA Wilaya ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiimba wimbo maalumu wa Michezo ya UMISSETA wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam Leo Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.

Maandalizi ya ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania yamezidi kupamba Moto katika Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es salaam.
Maandalizi hayo kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata timu ya Mkoa Wa Dar es salaam yameanza  Leo Mei 28, 2017 Kwa kuhusisha Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam ikiwemo Manispaa ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Kgamboni na Ubungo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Kwa ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam Kaimu Katibu Tawala katika upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno amewasihi washiriki kutumia weledi wao wa mafunzo waliyoyapata kuhusu michezo na kuonyesha umahiri wao ili kuchaguliwa katika timu ya Mkoa.
Wanafunzi hao ambao wameweka kambi katika Shule ya Sekondari Jitegemee mpaka Mei 31, 2017 wataanza safari ya kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano hayo ngazi ya Taifa yanayotaraji kuanza kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba June 6, 2017.
Otieno alisema kuwa vijana hao wanapaswa kutambua kuwa michezo ndio ajira inayolipa zaidi Duniani hivyo wanapaswa kudumisha nidhamu kwa kipindi chote Cha mashindano.
Aliongeza kuwa wanapaswa kutambua kuwa timu zote za Mkoa wa Dar es salaam zitakwenda Mwanza kushindana katika michezo hiyo ngazi ya Taifa na si kushiriki pekee.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo aliyezuru katika Uwanja wa Uhuru kujionea Timu ya Vijana wake kutoka Manispaa ya Ubungo ikichuana vikali na timu ya Manispaa ya Ilala amepongeza juhudi za washiriki wote ambao wameonyesha nidhamu ya Hali ya juu.
"Ukiona vijana Wana nidhamu Kama hivi ni vyena kuwapongeza na kuwatia moyo maana Bado Wana safari ndefu kimichezo na kimaisha" Alisema MD Kayombo
Mkurugenzi Kayombo ametilia msisitizo zaidi kutumia weledi wao ili kurejesha heshima ya michezo katika Manispaa ya Ubungo na Mkoa wa Dar es salaam Kwa ujumla.

Wednesday, 24 May 2017

CHATO WATAKIWA KUCHANGAMKIA KILIMO CHA MIHOGO CHENYE TIJA ILI KUINGIA KATIKA SOKO LA KIMATAIFA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) pamoja na wanahabari walipofika ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa mkoa huo leo.

Monday, 22 May 2017

ARSENAL YASHINDWA KUFUZU KWA MARA YA KWANZA KWA MIAKA 20

















Arsenal ilishinndwa kufuzu kwa kombe la klabu bingwa barani ulaya,  kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20 licha ya ushindi wake dhidi ya Everton wa mabao 3-1 katika siku ya mwisho ya mechi za Primia League.

Arsenal ilianza mechi vizuri ikiwa pointi moja nyuma ya Liverpool na walikuwa katika nafasi bora kuchukua nafasi yao wakati waliongoza mnamo dakika ya nane.

Lakini ukakamavu wa Liverpool uliiwezesha kusalia katika timu nne za kwanza baada ya kuwatandika Middlebrogh mabao 3-0.

Manchester City ilishika nafasi ya tatu baada ya kuinyuka Watfoird mabao 5-0.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube