Kwa kipindi kizima cha mwezi wa 5 (Mei) wateja wa DStv wamekuwa wakifurahia zaidi vipindi vyenye ubora na vya kusisimua vya Kiafrika.
Huba, Jikoni na Marion, Mchikicho wa Pwani, Yahusu Tanzania, Kimbembe ni kati ya vipindi kutoka Tanzania vilivyo bamba mwezi huu ndani ya chaneli Maisha Magic Bongo (DStv 160)
Meneja Mahusiano Multichoice Tanzania, Johnson Mshana amesema, “Mwezi Mei kwetu tumeufanya kuwa mwezi maalum kwa ajili ya kutangaza na kujivunia utajiri wetu waafrika ikiwa ni pamoja na utamaduni na Sanaa na michezo
Hii ni moja ya sehemu ya ahadi ya DStv kwa kutoa ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na burudani kwa kuendelea kusaidia Filamu za Afrika na kwa kuwekeza katika watu, mawazo na vipaji.
Ikiwa ni njia moja wapo ya kusheherekea mwezi huu wa Afrka, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania waliamua kuvaa mavazi maalum ya Kiafrika na kuandaa chakula maalum cha kiafrika kwa wafanyakazi wote.
Haikuishia hapo, Multichoice Tanzania pia imeandaa zawadi maalum za Kiafrika kwa waandishi wa habari, ikiwa ni njia ya kuonyesha shukrani kwa waandishi na kudumisha Umoja na Uafrika wetu.
#AFRIKAYETU
No comments:
Post a Comment