Timu ya vijana ya Serengeti Boy's inayoshiriki fainali za Matifa ya Afrika kwa umri huo huko Gabon usiku huu imewalazimisha sare ya bila kufungana mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mali.
Serengeti Boy's walicheza soka la kuvutia na pasi fupi fupi lakini safu ya ushambuliaji katika mchezo wa leo ilishindwa kupenyea katika ngome ya Mali, ambao safu yao nayo ilijaribu kupenya bila mafanikio.
Mchezo huo ulikuwa wakwanza kwa Serengeti ambapo sasa itakaa hadi Mei 18 watakapokutana na wapinzani wake wengine,Angola lakini mchezo wa leo ulikuwa mgumu kwa timu zote.
Kipindi cha pili Serengeti walicheza kwa tahadhari kubwa hususani safu ya ulinzi kupitia mabeki Nashon Naftal, pamoja na Ally Msengi walionekana kuwa mahiri huku kipa Kambwili akionyesha umhiri kwa kuokoa baadhi ya hatari.
No comments:
Post a Comment