Real Madrid ndio mabingwa wapywa wa Ligi Kuu nchini Uisspania La Liga baada ya kuibanjua Malaga kwa mabao 2-0 na kutwaa ubingwa wa La Liga.
Wachezaji wa Real Madrid wameony7esha furaha kubwa kwa kocha wao Mkuu Zinedine Zidane kwa mafanikio wanayopata kuptia yeye ambaye tangu amekuwa kocha amefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Ushindi huo kwa Zidane ni ushindi mkubwa kwa Mashabiki wa Real Madrid na sasa wanaamini ndiye mkombozi ambaye amevunja utawala wa soka kwa wapinzani wao Barcelona.
Kocha Zidane amenukuliwa akisema kuwa anajisikia furaha na kila muda maekuwa na muda mzuri wa raha katika msimu mzima uliopita wa Ligi na sasa anajiandaa kwa ajili ya fainali za Mabingwa Ulaya UEFA.
Madrid ilikua ikihitaji alama moja kabla ya mchezo huo walianza kupata bao la kuongoza katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Cristiano Ronaldo, kisha Karim Benzema akifunga bao la pili katika dakika ya 55.
Madrid wamemaliza msimu wakiwa na alama 93 kwa michezo 38 wakifuatiwa na mahasimu wao Barcelona waliomaliza na alama 90 baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Eibar.
No comments:
Post a Comment