BREAKING

Monday, 8 May 2017

NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa watoto (Toto Afya  Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.

Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.

“Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.

“Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.

Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.

“Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga  kwani itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.

Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo,Meneja huyo alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na katakuchangamkia fursa za mfuko huo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube