BREAKING

Tuesday, 16 May 2017

WANANCHI WA UHAMBILA ACHENI KUHARIBU VYANZO VYA MAJI NA MALIASILI ZENU

viongozi wa shirika la LEAT pamoja na viongozi wa kijiji cha Uhambila wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wakati wa kujadili maswala ya utunzaji wa Maliasili na vyanzo vya maji vilivyopo eneo hill.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kinachoendelea kwenye mkutano wa kijiji wa kujadili maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja Maliasili za kijiji hicho.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Wananchi wa kijiji cha uhambila wilayani Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na maliasili zilizopo katika kijiji hicho.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho Afisa mradi kutoka shirika la LEAT upande wa wilaya ya mufindi Jamali Juma alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujiepusha na ukataji miti hovyo na kulima vinyungu kwenye vyanzo vya maji kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha ukame.

"Mkiangalia zamani maeneo haya yalikuwa ya kijani na tulikuwa na mito midogo midogo mingi iliyokuwa inatililisha maji msimu mzima lakini hali ya sasa haipo hivyo kutokana na kutaka miti na kuaharibu vyanzo maji nawaomba wananchi acheni hiyo tabia ili tuwe na Mazingira mazuri kama zamani"alisema juma

Ukataji miti na uharibifu wa vyanzo unasababisha madhara mengi makubwa na ndio maana tunaona sasa kumekuwa na magonjwa mengi ambayo yanaathari ya moja kwa moja kwa mwanadamu lakini pia uharibifu huo husababisha mabadiliko ya vipindi vya mvua na kukosekana kwa mvua za kutosha.

Juma alisema kuwa dunia kwa sasa inakabiliana na swala la mabadiliko ya tabia nchi hata hivyo wananchi mnatakiwa kuwa umakini ili msije mkaishi kwenye jangwa kutokana na uharibifu wetu.

"Ni kosa la jinai kwa mtu yoyote yule kukata miti bila kibali au kuharibu vyanzo vya maji kutokana na sheria zetu za mwaka 1982 hivyo kukata miti au kuaribu vyanzo vya maji sio haki ya msingi ya mwananchi" alisema Juma

Shirika lisilo la kiserikali la Mwanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo( LEAT) wametoa elimu ya Mazingira kwa miaka minne mfululizo hivyo Vijiji vyote vya mradi ambavyo vipo wilaya ya iringa na wilaya ya Mufindi na kuiomba serikali kuendelea kuboresha Mazingira ambayo yapo chini yao.

Franklin Masika ni Afisa ughani wa shirika la LEAT aliwataka wananchi kufuata sheria ya mazingira mwaka 2004 namba 20  na sheria ya maji ya mwaka 2009 namba 11 zinaeleza wazi kuhusu kilimo cha vinyungu au kulima kandokando ya mto au kwenye vyanzo vya maji na kuna faini zimeolodhishwa hivyo sheria hizi sio ngeni ili zilikuwa hazifuatwi lakini saizi serikali imeanza kuzifuatilia kwa umakini zaidi.

"Mkiangalia nyie hapa kijiji cha uhambila kipo katika bonde la mto rufiji hivyo wananchi mnatakiwa kuwa makini na hizi sheria kwa kuwa lengo la serikali ni kuboresha Mazingira ya kuukuza mto ruaha mkuu ambao unahati hati ya kutoweka na nyie ni walinzi namba moja wa Mazingira "alisema Masika

Lakini Franklin Masika aliztaja baadhi ya adhabu zinazotokana na uharibifu wa Mazingira mfano kuchepusha maji,kukinga,kuchukua au kutumia maji kinyume cha sheria ni kosa la jinai na adhabu yake ni shilingi 300,000 na isiyozidi 500,000 au kifungo cha miezi miwili na kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na hizo sheria.

Masika aliwataka wananchi wa kijiji cha uhambila kuwa kutunza vyanzo vya maji na Mazingira kwa ujumla ili kuboresha maeneo wanayoishi na kupunguza au kufuta Kabisa milipuko ya magonjwa ilanayotokea mara kwa mara katika maeneo ya Vijijini.

Chelsoni Kikoti, Amani Nyakunga na Reginandi Chalamila ni wananchi wa kijiji cha uhambila  waliiomba serikali zitafakali upya sheria hizo kwa kuwa zinawaumiza wananchi wa vijijini kutokana na Mazingira wanayoishi kutokuwa rafiki na namna ya kupata kipato hivyo wemekuwa wakitegemea sana kilimo cha mboga mboga kuendesha maisha yao.

"Hebu angalieni Mazingira haya tunayoishi hakuna njia nyingine ya kupata kipato zaidi ya kutegemea kulima vinyunguni ambako tunalima mboga mboga tu jamani hee tuatakufa na njaa hebu muishauri serikali juu sheria hizo"walisema wananchi

Thomas Mtelega afisana mradi wataasisi ya mufindi kwa maendeleo (MUVIMA) aliwaomba wananchi kulima Kilimo cha kisasa kutokana na Mazingira wanayoishi na kuacha tabia za kukata miti pamoja na kuharibu vyanzo vya maji mfano kulima mboga mboga ni rahisi unaweza kulima hata kwa kutumia maji.

"Kuna maji machafu ambayo tunayoyatumia majumbani kwetu ni maji ambayo tunaweza kuyatumia katika Kilimo cha mboga mboga kwa kuchukua udongo na kuuweka kwenye gunia au visarufeti ambavyo ukipanda mbegu unaweza kupata mboga nzuri na salama kwa kuwa guni au kisarufeti kinaweza kujchuja uchafu wote na kuiacha mboga ikiwa salama hivyo nawashauri wananchi kutumia njia hii ili kuondokana na ulimaji wa karibu na vyanzo vya maji na kusababisha Mazingira yanaboresha na kuwa mazuri"alisema Mtelega
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha uhambila Agnes Simba aliwashukuru shirika la LEAT kwa elimu waliyokuwa wanantoa kwa miaka nne ambayo imewakomboa wananchi kwa kupata vitu vingi ambavyo sasa vimeanza kutokea na vinakuwa sio vigeni hasa maswala ya sheria za Maliasili na utunzaji wa vyanzo vya maji ambavyo vinafaida kwa wananchi wa sasa na baadae.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube