Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale kulia akimueleza jambo Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kushoto wakati alipofungua maonyesho ya tano ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania (TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara kimataifa.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Augustino Kasale akizungumza na waandishi wa habari leo
MRADI wa Bomba
la
Mafuta Mkoani Tanga umefikia kwenye hatua ya wataalamu kukagua njia
itakayopitisha miundombinu ya bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga.
Hatua hiyo
imekuja
baada ya serikali ya Tanzania na Uganda kutiliana saini ya mkataba baina ya
nchi na nchi (Iga) kukamilika.
Hayo yalisemwa
leo na
Mwanasheria Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini Tanzania
(TPDC), Kelvin Gadi wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao
ambalo lipo eneo la mwahako jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya
biashara kimataifa.
Alisema tayari
wameshafanya maamuzi yameshakamilika wataalamu wanafanya tathimi ya udongo
katika njia ambayo bomba hilo litapita kwa taarifa ya awali njia iliyopatikana
upana mita 200 na baadae watalaamu wataipunguza mpaka
100.
Awali
akizungumza
kuhusiana na mradi huo, Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Augustino Kasale alisema
mradi huo utapita katika mikoa nane ya Tanzania na kuzalisha ajira 10000 za
kudumu na muda mfupi.
Alizitaja fursa
ambazo zitakuwa moja kwa moja ni hutoaji huduma wakati wa ujenzi, ajira za muda
mfupi na moja kwa moja, fursa za usafirishaji ikiwemo kuufungua mkoa wa Tanga
kiuchumi.
“Hivyo hivi sasa
wananchi
wa mkoa wa Tanga wanapaswa kujiandaa na ujio wa Bomba la Mafura ghafi
kutoka hoima
nchini Uganda hadi Mkoani Tanga “Alisema.
No comments:
Post a Comment