Wazalishaji wadogo wadogo wa
bidhaa nchini wameshauriwa
kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la
Viwango Tanzania TBS.
Hayo
yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes
Kaseka pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari
kwenye maonyesho ya tano
ya biashara ya Mkoa wa Tanga .
Alisema
kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na
wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha
kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora.
"Bado
wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza
kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza
kuingiza bidhaa zao kwa urahisi katika masoko ya ushindani tofauti na
sasa" alisema Kaseka.
Aidha
alisema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanaziondosha
katika soko bidhaa ambazo ni hafifu kwa kufanya ukaguzi wa Mara kwa Mara
katika masoko na maeneo yote yanayohusika na shughuli za uuzaji wa
bidhaa.
Nae
Mfanyabiashara Aisha Kisoki alisema kuwa changamoto kubwa ni muingiliano
wa bidhaa kutoka nje ambazo kwa hapa nchini zinauzwa kwa bei rahisi
tofauti na wanazozizalisha.
Alisema
kuwa iwapo TBS wataweza kudhibiti uingiaji usio rasmi wa bidhaa kutoka
nje utasaidia sana wafanyabiashara wa ndani ya nchi kuona umuhimu wa
kuweka nembo bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment