Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 amefanya mazungumzo na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakifatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg john Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 wakati wa kika na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa
Paul C. Makonda akisisitiza jambo
Imebainika kuwa zipo kauli zisizo rafiki zinazotolewa Na watumishi wa Umma dhidi ya wananchi katika Jiji la Dar es salaam wanaozuru katika Ofisi mbalimbali kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali kutokana Na mambo yanayowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda amebainisha hayo Leo Mei 18, 2017 Wakati akizungumza Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambapo pia ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.
Mhe Makonda amesema kuwa mtumishi wa serikali ambaye atabainika kutumia lugha ambazo sio rafiki kwa wananchi atachukuliwa hatua za kinidhamu Mara baada ya kubainika kwani kufanya hivyo ni kufifisha uaminifu wa wananchi dhidi ya serikali.
Sambamba Na hayo pia RC Makonda amesema kuwa Kazi ya watendaji serikalini ni kutatua kero za wananchi japo wapo watendaji ambao wamegeuka Na kuanza kuongeza migogoro badala ya kutatua.
Alisema kuwa baadhi ya watumishi wa Sekta ya ardhi wanamiliki kampuni zinazojihusisha Na mambo ya Ardhi Jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likipunguza ufanisi katika utendaji kwani wanatumia muda mwingi kufikiri kuhusu kampuni zao kuliko kuwatumikia wananchi serikalini.
Ametoa wiki moja kwa watumishi wote wanaomiliki kampuni hizi kuamua moja ama kubali wakifanya Kazi serikalini Na kuachana Na kampuni binafsi ama kubakia katika kampuni zao Na kuacha kazi serikalini.
"Watumishi hawa hutumia vifaa vya serikali kwenye miradi yao Jambo ambalo hupelekea uchakavu Na uharibifu wa haraka wa vifaa vya serikali hivyo zuio langu hili linajikita kuwataka watumishi wa Umma katika Mkoa wangu kujikita katika utendaji wa shughuli za serikali" Alisema Mhe Makonda
Alisema Ardhi Na Ujenzi ni moja Kati ya Idara zenye matatizo mengi katika Mkoa wa Dar es salaam hivyo ametoa msisitizo vibali vya Ujenzi kutolewa haraka ndani ya mwaka mmoja kwani kuchelewesha kunapelekea wananchi wengi kujenga bila utaratibu.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia kwa watendaji wa Sekta hiyo ya Ardhi Na Ujenzi ambayo ni pamoja Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu, Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017 huku Mwanzoni mwa mwezi wa Saba kukitarajiwa kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.
Wakuu wa Idara katika Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano Na waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari, kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, Na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo, kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama vile Shule, Hospitali, Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba Na kutoa Mikakati wa Upimaji.
Maelekezo mengine ni pamoja Na Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha ufanisi Na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi, Kushughulikia changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa Upimaji Na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka Na Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa Na utendaji imara unaoshabihiana Na Jambo la kisera.
Pia Kila Mtumishi kufanya Kazi yake kwa Uaminifu kwani dhamana aliyopewa ni kubwa Na anapaswa kuitendea Haki, Watumishi wote kusimamia Na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba Na wananchi katika kipindi cha miaka mitano, Kila Mkuu wa Idara kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba Na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma Na kuielewa vyema ilani hiyo.
Kufatilia Na kufahamu upandaji wa madaraja Na stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja Na kwenda likizo, Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo Na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika, Kuwa Na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi Na Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha Na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume Na sheria. Na endapo wasipojitokeza Na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.
RC Makonda pia ameelekeza wakuu wa Idara Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa Sambamba Na kutoogopa maadhimio kama wanatenda Kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo kupendelea, Wakuu wa Idara kila.
No comments:
Post a Comment