BREAKING

Thursday, 18 May 2017

TIMU YA TAIFA YA VIJANA SERENGETI BOYS YAICHARAZA MABAO 2-1 ANGOLA



Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 Serengeti boys imeendelea kutisha katika kandanda katika Fainali za Mataifa ya Afrika baada ya hii leo kuichapa mabao 2-1 timu ya Vijana ya Angola

Vijana hao waliotandaza soka la kitabuni walianza kupata bao mapema kwa ushirikiano mzuri wakigongeana pasi fupi fupi huku wakicheza kwa kiwango cha juu na kuwafanya wapinzani wao kujulinda zaidi.

Angola baada ya kuona vijana wapo katika umakini zaidi kimchezo walicharuka nao wakarejesha bao na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1, kipindi cha pili waliporejea vijana hao walitesa zaidi kwani walishambulia kila wakati lango la wapinzani wao na hatimaye wakafanikiwa kupata bao la ushindi likifungwa kwa ufundi mkiubwa.

Baada ya kuopata bao hilo Serengeti boys hawakubweteka kwani walizidi kuwashambulia wapuinzani wao ambao walizidiwa kwa kila idara katika mchezo wa leo.

Kwa matokeo hayo Serengeti Boys wamepanda kileleni mwa kundi lao kwa kufikisha pointi 4 na kuziacha timu za Mali, Niger Angola nyuma, huku mchezo mwingine utapigwa usiku huu kati ya Mali na Niger.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube