Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(MB) akimsikiliza Mbunge wa Iramba Mashariki Mheshimiwa Allan Kiula wakati walipo kutana katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Waziri Mkuu yupo Mkoani Dodoma katika kushiriki Mkutano wa Sita wa Bunge la Kumi na moja amabao umeanza leo Tarehe 31 January 2017
Tuesday, 31 January 2017
MHANDISI MTIGUMWE AWAONDOA HOFU WATUMISHI KUHAMIA DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo
Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe
Mhandisi Mtigumwe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu cha kuhusiana na uamuzi wa serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi mkoani Dodoma kilichokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea mjini Dodoma.
Mtigumwe amebainisha kuwa Awamu ya Kwanza ya uhamisho utawahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, ambapo katika mchakato huo watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia tarehe 14 – 15/2/2017 na wengine 47 waliobaki watahamia muda wowote katika kipindi cha kuanzia mwezi Februari hadi kufikia mwezi Juni.
Mtigumwe amewaeleza watumishi hao kuwa maandalizi ya ofisi za Wizara ya kilimo zilizopo mjini Dodoma zinaendelea vizuri na tayari baadhi ya maeneo yamekamilika huku mengine yakiendelea kukamilishwa ili kukidhi matakwa kwa ajili ya watumishi wote watakapohamia mjini Dodoma.
Uamuzi wa Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuhamia mjini Dodoma ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Serikali yote kuhamia Dodoma ili kutekeleza uamuzi uliofikiwa tangia miaka ya 70 na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutambua na kutangaza kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.
Mhandisi Mtigumwe amebainisha hayo hii leo katika kikao cha pamoja na watumishi wa wizara ya kilimo katika Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii
leo amewaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuhusu zoezi la serikali kuhamia
Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za
utumishi wa Umma.
Mhandisi Mtigumwe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu cha kuhusiana na uamuzi wa serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi mkoani Dodoma kilichokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea mjini Dodoma.
Mtigumwe amebainisha kuwa Awamu ya Kwanza ya uhamisho utawahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, ambapo katika mchakato huo watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia tarehe 14 – 15/2/2017 na wengine 47 waliobaki watahamia muda wowote katika kipindi cha kuanzia mwezi Februari hadi kufikia mwezi Juni.
Mtigumwe amewaeleza watumishi hao kuwa maandalizi ya ofisi za Wizara ya kilimo zilizopo mjini Dodoma zinaendelea vizuri na tayari baadhi ya maeneo yamekamilika huku mengine yakiendelea kukamilishwa ili kukidhi matakwa kwa ajili ya watumishi wote watakapohamia mjini Dodoma.
Uamuzi wa Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuhamia mjini Dodoma ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Serikali yote kuhamia Dodoma ili kutekeleza uamuzi uliofikiwa tangia miaka ya 70 na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutambua na kutangaza kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.
Mhandisi Mtigumwe amebainisha hayo hii leo katika kikao cha pamoja na watumishi wa wizara ya kilimo katika Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
09:05
JUMA PONDAMALI 'MENSA' AELEZA HISTORIA KALI YA SOKA TANGU AKIWA NA UMRI WA MIAKA 13, UNAMKUMBUKA? TAZAMA VIDEO NA MAHOJHIANO YAKE
Mcheza soka
mkongwe hapa nchini maarufukama Juma Pondamali “Mensa” ambeye kwa sasa ni kocha
wa “Young Africa” amefunguka mbelea ya Super News Tv Online na kumtaja kocha
ambaye alimkuza kisoka toka akiwa mdogo yaani umri wa miaka 13-14.
Juma
Pondamali alikuwa ni golikipa hodari aliye fanikiwa kuiwakilisha Tanzania miaka
ya 1980 katika michuano ya “African Cup of Nation”.
Tumia dakika
zako kadhaa kuitaza hii video ili ujue mengi kuhusu Nyota huyo. Endelea kutufuatilia hapa soon tutakuletea
Taarifa yake mpya ya kuachia wimbo wake wa singeli…..
09:03
Monday, 30 January 2017
MABINGWA WA AFRIKA KLABU YA MAMELODI SUNDOWNS WATUA NCHINI, KUUMANA NA SIMBA PAMOJA NA AZAM FC
Klabu Mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wametua jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya vigogo wa Tanzania, Simba na Azam FC .
Timu hiyo imewasili ikiwa na msafara wa takribani watu 50, ambapo 25 miongoni mwao ni wachezaji ambao watasakata kandanda na timu hizo za Simba na Azam FC.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Pitso Mosimane, pamoja na Nahodha Hlompho Kekana,wamesema ujio wao ni kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.
Wamesema kuwa wanaamini timu hizo zinaushindani mkubwa kisoka hivyo watapata mazoezi ya kutosha katika micvhezo hiyo miwili.
Mchezo wa kwanza utachezwa Februari 1 na wa pili utakuwa Februari 3 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
19:16
WAZIRI MKUU AKIFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA RCC MKOA WA DODOMA
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akihutubia leo wakati wa kufungua baraza la ushauri (RCC) Mkoa wa Dodoma ambapo lilishirikisha Wizara,Idara na Wadau mbalimbali wanaoratibu ujio wa Serikali kuhamia Makao makuu Dodoma Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma
19:07
Friday, 27 January 2017
SERIKALI YAWAFUNGULIA SIMBA, UWANJA WA TAIFA SASA KUANZA KUTUMIKA KESHO,AZAM FC KUKIPIGA NA SIMBA TAIFA
SERI
Serikali imeufungulia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na imeruhusu mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC na Simba uchezwe hapo kesho.
Simba watakuwa wenyeji wa Azam FC kesho katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mchezo huo utafanyika rasmi Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru, Dar es Salaam kufuatia tamko la Serikali .
Afisa Habari wa Simba Hajji Manara amedhibitisha hilo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya soka Tanzania TFF ambapo amesema kuwa Serikali imewaachia kuutumia Uwanja wa taifa akisema ni jambo jema na linaonyesha nia njema ya kukuza soka nchini.
Amewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuzingatia nidhamu ndani ya uwanja huo, kwani iwapo mwanachama na shabiki yoyote atafanya jambo kinyume na maadili atachukuliwa hatua kali kwa kuwa sasa uongozi wa klabu umeamua kulivalia njuga suala la nidhamu kwa mashabiki.
Taaruifa za awali zilizotolewa na Zawadi Msalla, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali zimesema kwamba Uwanja huo unafunguliwa baada ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kujiridhisha na ukarabati uliofanywa baada ya uharibifu uliosababishwa na tukio la Oktoba 1, mwaka jana kati ya mechi ya Simba na Yanga iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo huo kulitokea vurugu baina ya mahasimu,hao na kuvunja viti, baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu.
Tambwe alifunga bao lake dakika ya 26, akimalizia pasi ya beki Mbuyu Twite na kufunga lakini mashabiki hawakukubaliana na bao hilo baada ya wachezaji wa Simba kumvaa mwamuzi Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.
Katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa madai ndiye aliyekuwa mstari wa mbele, kuleta vurugo, ambapo baadae Mkude alifutiwa kadi hiyo na Saanya kufungiwa miaka miwili kuchezesha.
15:26
Thursday, 26 January 2017
ZIARA YA MAJALIWA MGODI WA LIGANGA - LUDEWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi la Shirika la Maendeleo la Taif (NDC), Samuel Nyantahe baada ya kuwasili kwenye ueneo la mgodi wa Liganga wilayani Ludewa kukagua maendeleo ya hatua muhimu zitakazowezesha kazi uchimbaji chumakuanza haraka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Eric Mwingira kuhusu sampuli ya chuma kilichogunduliwa katika mgodi wa Liganga wakati alipotembelea mgodi huo Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea mgodi wa chuma wa Liganga wilaya Ludea Januari 26, 2017. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mlima wenye mwamba ambao watalaamu wa madini wameeleza kuwa kwa zaidi ya asilimia 60 una madini ya chuma katika eneo la Liganga lililotembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilaya Ludea januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikaguaeneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa januari 26, 2017. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mlima utaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea mgodi wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa Januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wanawake wa kijiji cha mundindi wilayani Ludewa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia baada ya kukagua mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Eric Mwingira kuhusu sampuli ya chuma kilichogunduliwa katika mgodi wa Liganga wakati alipotembelea mgodi huo Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea mgodi wa chuma wa Liganga wilaya Ludea Januari 26, 2017. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilaya Ludea januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikaguaeneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa januari 26, 2017. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mlima utaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea mgodi wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa Januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wanawake wa kijiji cha mundindi wilayani Ludewa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia baada ya kukagua mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mundindi wialyani Ludewa baada ya kutembelea mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
18:46
Monday, 23 January 2017
DK. KIGWANGALLA ASHIRIKI MAULIDI YA KUADHIMISHA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD(SAW) DAR
N
Mbali na Dk. Kigwangalla, wageni wengine ni pamoja na Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega huku kwa viongozi wa dini walikuwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa ambapo wote kwa pamoja walipewa zawadi maalum na kampuni hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali katika tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na wageni waalikwa wengine katika tukio hilo akiwemo Prof. Ibrahim Lipumba
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni katika hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
Baadhi ya vijana wa Madrasa mbalimbali kutoka Dar es Salaam na baadhi ya mikoa wakifuatiliatukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Naibu waziri wa Tamisemi, Mh. Suleiman Jafo wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na Naibu waziri wa Tamisemi wakati wakiwasubiria wageni waalikwa akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakati wa kumpokea alipowasili kwenye hafla hiyo.
dua zikiendelea
Dua zikiendelea
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi, akizungumza katika tukio hilo
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea zawadi kwenye hafla hiyo.
Dk. Kigwangalla akipokea zawadi katika hafla hiyo
09:02
Subscribe to:
Posts (Atom)