BREAKING

Tuesday 29 November 2016

RAIS LUNGU WA ZAMBIA AONDOKA NCHINI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na watatu kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi John Kijazi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Rais John Magufuli akiongozana na  mgeni wake, Rais Edgar Chagwa Lungu wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu wakishuudia wakati Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu akiagana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kabla ya kuondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais John Magufuli akiagana na Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere wakati mgeni huyo alipoondoka nchini kurejea nyumbani Novemba 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Rais John Magufuli akiwapungia wananchi waliojitokeza kumuaga Rais wa Zambia, Edgar Chagwa Lungu kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere wakati alipoondoka nchini kurejea nchini Novemba 29, 2016. Wengine pichani ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


RC SINGIDA AANZA ZIARA KUTEMBELEA KATA 136 ZA MKOANI SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe katika ziara yake katika Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Godfrey Mwambe akiongea na wananchi katika ziara ya mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew J. Mtigumwe

Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo ameanza ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkoa wa Singida.

Rc Mtigumwe ameanza ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Itigi, iliyopo katika Wilaya ya Manyoni ambapo atatembelea kata zote za halmashauri hiyo.

Pamoja na kutambua kero za wananchi na mambo mengine pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida anatumia mikutano hiyo maalumu kwa ajili ya kufahamiana na wanachi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero zao ambazo zimewasua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.

Mtigumwe akiwa katika Kijiji cha Doroto amehimiza zaidi wananchi kuandaa vyema mashaba yao na kuzingatia kilimo chenye kustahimili ukame kwani kuna mabadiliko makubwa ya tabia nchi jambo ambalo limepelekea kuchelewa kuanza kwa mvua.

Mhe Mtigumwe amewaagiza maafisa kilimo wa Kata na Wilaya zote za Mkoa wa Singida kutokaa ofisini kipindi hiki cha msimu wa kilimo badala yake kwenda mashambani kuwasaidia wananchi mbinu bora za kilimo sambamba na kuwasaidia namna bora ua kuandaa mashamba.

Sambamba na hayo pia amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo watakayopatiwa na Maafisa kilimo ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi zaidi kwa kilimo chenye tija.

Katika ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Singida.

KINANA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA CPC CHINA

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (Wakwanza kushoto),  alipokutana naye na kufanya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. Wapili ni Kaimu Balozi wa China hapa Nchini, Gou hao Domg. Na walioketi kulia, ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Katibu wa NEC, Sisa na Ushorikiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chama. 

Monday 28 November 2016

MAJALIWA AKISALIMIANA NA RAIS WA CHAD


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Chad , Idriss Deby Itno  baada ya Rais huyo kuwasili nchini Novemba 27, 2016.  Katikati ni Makamu wa Rais Samia Suluhu. (Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZIARA YA MAKONDA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KINONDONI YANOGA LEO, AKATIZA VICHOCHORO KUSAKA KERO, ACHAPA KAZI KIKAMILIFU NA AFANDE SIRRO, AMTUMBUA MGANGA MKUU


 TUCHAPE KAZI KIONGOZI: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwaga kicheko na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mkoa huo, walipokuwa wkijadili jambo, baada ya kuzungumza na viongozi na watendaji kutoka wilaya ya Kinondoni, katika Bwalo na Maofisa wa Polisi, Msaki mwanzoni mwa ziara yake katika mkoa wa Dar es Salaam, leo. Zifuatazo ni taswira katika picha kama alivyowanasa Mmiliki wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo aliyekuwa katika ziara hiyo.



  




 TANDALE
🔻
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua chumba cha biashara cha Mamalishe (kushoto), aliyemkuta akiwa kazini eneo la Tandale, akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Makonda akimwangalia mamalishe huyo wakati akiandaa chakula 
 Makonda na msafara wake wakikatiza mitaa ya Tandale wakati akisaka kero za wananchi wakati wa ziara hiyo ya aina yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wanne ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
 Salum Ali Hapi akimpa maelezo Makonda walipofika kukagua eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo Tandale, Kata ya Manzese
 Makonda akizungumza na wateja wa pombe za kieyeji aliowakuta katika kwenye kilabu cha pombe hizo, eneo la Uwanja wa Fisi
Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Mandela akikata funda la pombe ya kienyeji mbele ya Makonda bila wasiwasi kuwa yupo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  
 Makonda akijaribu kupiga hodi kwenye moja vya vyumba inayoelezwa kuwa ni ya madanguro ya ukahaba katika eneo hilo la Uwanja wa Fisi. Pamoja naye ni Hapi na Sirro 
 Kamanda Sirro naye akijaribu kumsaidia Makonda kupisha hodi lakini pia bila mafanikio ya kuitikiwa na waliokuwa wamejifungia ndani 
 Makonda akichukua bia kutoka kwa mhudumu wa baa pekee aliyoikuta wazi wakati myinge zote zikiwa zimefungwa kuhofia ujio wake.
 Makonda akiitazama kwa makini bia hiyo kuona tarehe yake ya mwisho wa matumizi, ili kujiridhisha kwa kuwa huelezwa kwamba baa zilizopo eneo hilo la Uwanja wa Fisi huuza vinywaji hadi vilivyokwisha mda wake wa matumizi. Bia hiyo aliikuta bado inafaa kwa matumizi.


 SHULE
 Makonda akitazama paa la chumba cha darasa katika shule ya Msingi Tandale, lililoporomoka wakati wa upepo mkali ulioambatana na mvua


MIUNDOMBINU YA BARABARA
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitazama majitaka yakitiririka kwenye daraja la barabara kutoka Tandale kwenda Mwananyamala. Makonda aliahidi barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami, la kwamba kabla ya hatua hiyo itafanyiwa matengenezo ya awali kuziba makorogoro ili iweze kupitika. 
 Makonda akipita pembeni pembeni kukwema maji machafu yaliyotuama kwenye sehemu ya barabara hiyo
 Mara huyu mama naye akamvaa na kumweleza kero zake wakati akipita

MKUTANO UWANJA WA SHULE YA MSINGI TANDALE

 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi akimkaribisha Makonda kuanza kuunguruma ili kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu papo hapo au baadae, katika mkutano wa hadhara uliofayika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Tandale, leo
 Makonda akizungumza 
 Makonda akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta.
 Umati wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akifuatilia jambo kwenye simu yake wakati wa mkutano huo. Mpogolo ni miongoni mwa waratibu wa ziara hiyo ya siku kumi ya Makonda katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.
 Watu wa huduma ya kwanza wakimpeleka kwenye gari ili kupelekwa haraka hospitali baada ya kuangua wakati wa mkutano huo
 Akiingizwa kwenye gari la wagonjwa la Manispaa ya Kinondoni
 Wananchi kwenye mkutano huo
 Makonda akianza kujibu kero kwa kuwahoji watendaji kulingana na wananchi walivyotaka kujibiwa kero husika.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya (aliyeshika kinasa sauti), akisubiri hukumu ya Makonda baada ya kushindwa kueleza ikiwa alikuwa anajua au hajui kadhia ya dawa kuibwa mara kwa mara katika Zahanati ya Tandale kama wananchi walivyolalamika, ambapo alisema hajui
" Haiwezekani uwe Mganga Mkuu wa Wilaya katika mkoa wangu halafu hujui kuhusu kuibwa kwa dawa kwenye zahanati, hii haikubaliki, kuanzia sasa si mganga Mkuu wa Kinondoni, Nitawaambia wizara inayokuhusu wakupangine wilaya katika mikoa mingine ambako watavumilia uzembe kama papo", alisema Makonda wakati akimtumbua Msuya kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika shule ya Msingi Tandale. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO- theNkoromo Blog

Friday 25 November 2016

BAADA YA KUTANGAZWA KUWA KOCHA MKUU MPYA WA YANGA, GEORGE LWANDAMINA AMESEMA HANA MPANGO WA KUFANYA MABADILIKO KATIKA BENCHI LA UFUNDI

 Kocha Lwandamina akikumbatiana na Mkurugenzi mpya wa Yanga Pluijm
wakati wa Utambulisho wa Benchi jipya la Ufundi 



Klabu ya soka ya Yanga imemtangaza rasmi Mzambia George Lwandamina kuwa kocha Mkuu mpya, ambaye sasa atachukua mikoba iliyoachwa na mholanzi Hans Van Der Pluijm.

Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, ya Yanga , Dar es Salaam wakati wa utambulisho huo  Lwandamina amesema kwamba hana mpango wa kubadilisha chochote kwenye benchi la Ufundi.

Lwandamina akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari juu ya kuongeza wachezaji amesema kwamba ameiona Yanga katika mechi yake ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikishinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na amegundua ni timu nzuri ambayo haihitaji mchezaji mpya.

Aidha ametoa pongezi kwa mtangulizi wake, Pluijm kwamba amefanya kazi nzuri akihaidi kufuata nyayo zake na atashirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha Yanga inapata mafanikio zaidi.

Aidha Lwandamina amekana madai kwamba amependekeza wachezaji wawili aliokuwa nao Zesco United ya kwao, Zambia kiungo Misheck Chaila na mshambuliaji Mkenya Jesse Were wasajiliwe .

 Kwa upande wake aliyekuwa kocha wa Yanga ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Benchi jipya la Ufundi Yang Hans Van  Pluijm amesema kwa ufupi kuwa amefanya kazi na Yanga kwa kiwango kikubwa akiwa kocha ikiwepo kucheza jumla ya mechi 128 kwenye awamu mbili, akishinda 80, sare 25 na kufungwa 23,na katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amemsifu kocha huyo wa zamani kwa kumelezea alifanya kazi kubwa yenye kuheshimiwa jambo lilolowasukuma kumpa ukurugenzi wa Benchi la Ufundi.

Wednesday 23 November 2016

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA SITA WA TUCTA MJINI DODOMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama   (watatu kulia), Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana  (wapili kulia) na Rais  wa  Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Gratian Mukoba (kulia) wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufungua Mkutano Mkuu wa  Sita wa  TUCTA, Novemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Sita wa  Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA) wakiimba wimbo wa Mshikamano kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua mkutano wao kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi, Angela Kairuki akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri )

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUKTA) kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Novemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube