BREAKING

Friday 25 November 2016

BAADA YA KUTANGAZWA KUWA KOCHA MKUU MPYA WA YANGA, GEORGE LWANDAMINA AMESEMA HANA MPANGO WA KUFANYA MABADILIKO KATIKA BENCHI LA UFUNDI

 Kocha Lwandamina akikumbatiana na Mkurugenzi mpya wa Yanga Pluijm
wakati wa Utambulisho wa Benchi jipya la Ufundi 



Klabu ya soka ya Yanga imemtangaza rasmi Mzambia George Lwandamina kuwa kocha Mkuu mpya, ambaye sasa atachukua mikoba iliyoachwa na mholanzi Hans Van Der Pluijm.

Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, ya Yanga , Dar es Salaam wakati wa utambulisho huo  Lwandamina amesema kwamba hana mpango wa kubadilisha chochote kwenye benchi la Ufundi.

Lwandamina akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari juu ya kuongeza wachezaji amesema kwamba ameiona Yanga katika mechi yake ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikishinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na amegundua ni timu nzuri ambayo haihitaji mchezaji mpya.

Aidha ametoa pongezi kwa mtangulizi wake, Pluijm kwamba amefanya kazi nzuri akihaidi kufuata nyayo zake na atashirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha Yanga inapata mafanikio zaidi.

Aidha Lwandamina amekana madai kwamba amependekeza wachezaji wawili aliokuwa nao Zesco United ya kwao, Zambia kiungo Misheck Chaila na mshambuliaji Mkenya Jesse Were wasajiliwe .

 Kwa upande wake aliyekuwa kocha wa Yanga ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Benchi jipya la Ufundi Yang Hans Van  Pluijm amesema kwa ufupi kuwa amefanya kazi na Yanga kwa kiwango kikubwa akiwa kocha ikiwepo kucheza jumla ya mechi 128 kwenye awamu mbili, akishinda 80, sare 25 na kufungwa 23,na katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amemsifu kocha huyo wa zamani kwa kumelezea alifanya kazi kubwa yenye kuheshimiwa jambo lilolowasukuma kumpa ukurugenzi wa Benchi la Ufundi.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube