Manchester United na Arsenal zimetoshana nguvu sawa katika mchezo wao baada ya kutoka sare ya bao 1-1, lakini mchezo huo licha kuwa wa kuonyesha unaupinzani mkubwa uwanjani,upinzani mwingine bado upo kwa mameneja wa tyimu zote hizo mbili.
Jose Mourinho na Arsene Wenger wanaonekana bado hawaivi chungu kimoja tangu walivyoanza kurushiana maneno miaka kadhaa iliyopita.
Katika mchezo wa leo mara baada ya mechi ya o kumalizika makocha hao walipeana mkono kila mmoja akiwa ameangalia upande mwingine kabisa inshara inayoashiria kuwa mambo si mazuri
walipeana mkono kama sehemu ya kutimiza kile kinachoweza kuitwa bora liende huku kila mmoja akitazama nanapopajua.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1,Arsenal wakilazimika kusawazisha bao likifungwa kwa kichwa na Mfaransa Olvier Giroud akitokea benchi.
No comments:
Post a Comment