BREAKING

Tuesday, 29 November 2016

RC SINGIDA AANZA ZIARA KUTEMBELEA KATA 136 ZA MKOANI SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto
 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe katika ziara yake katika Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Godfrey Mwambe akiongea na wananchi katika ziara ya mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew J. Mtigumwe

Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo ameanza ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkoa wa Singida.

Rc Mtigumwe ameanza ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Itigi, iliyopo katika Wilaya ya Manyoni ambapo atatembelea kata zote za halmashauri hiyo.

Pamoja na kutambua kero za wananchi na mambo mengine pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida anatumia mikutano hiyo maalumu kwa ajili ya kufahamiana na wanachi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero zao ambazo zimewasua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.

Mtigumwe akiwa katika Kijiji cha Doroto amehimiza zaidi wananchi kuandaa vyema mashaba yao na kuzingatia kilimo chenye kustahimili ukame kwani kuna mabadiliko makubwa ya tabia nchi jambo ambalo limepelekea kuchelewa kuanza kwa mvua.

Mhe Mtigumwe amewaagiza maafisa kilimo wa Kata na Wilaya zote za Mkoa wa Singida kutokaa ofisini kipindi hiki cha msimu wa kilimo badala yake kwenda mashambani kuwasaidia wananchi mbinu bora za kilimo sambamba na kuwasaidia namna bora ua kuandaa mashamba.

Sambamba na hayo pia amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo watakayopatiwa na Maafisa kilimo ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi zaidi kwa kilimo chenye tija.

Katika ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube