Hatimaye Kocha George Lwandamina amemalizana na klabu ya Zesco ambayo ameipa mafanikio makubwa tangu ajiunge nayo .
Kocha huyo ambaye siku chache alikuwa nchini na kuleta mtikisiko kwa kocha aliyepo Han ameachia ngazi rasmi kuinoa Zesco ambayo mkataba wake ulikuwa unaisha Januari 2017.
Lwandamina amethibitisha kuachia ngazi katika klabu hiyo, kwa taarifa yake mwenyewe .
"Ni kweli, tumemalizana vizuri kabisa na mambo yamekwenda kitaalamu," alisema.
Kuhusiana na kutua Yanga, Lwandamina amekubali kuwa anakuja nchini lakini hakutana kuweka wazi.
"Baada ya hapa Zesco, sasa naelekea katika nchi nyingine ya Afrika. Nipe siku moja nikupe jibu," alisema.
Lakini taarifa za uhakika zinaeleza kwamba kocha huyo atafika nchini kesho usiku kwa ajili ya kumalizana na Yanga.
"Tunajua anakuja huko Tanzania kesho usiku, ndege yake inaonyesha hivyo," alisema wakala wake.
No comments:
Post a Comment