Rais wa zamani wa shirikisho la Soka Tanzania 'TFF' na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga amemwelezea aliyekuwa Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Muhammad Abeid aliyefariki dunia jana jioni katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, kuwa alikuwa mpenda michezo na asiyekuwa na maneno ya kukatisha tamaa.
Tenga ameeleza hayo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema katika vikao vyote ambavyo alikuwa akiingia juu ya kujadili mstakabali wa vilabu alikuwa kiongozi na mwenye kutatua matatizo ya vilabu hususani pale lilipokuja suala la Bodi ya Ligi kwa kuwa alikuwa anahusika kwa kiasi kikubwa.
Amesema kuwa Marehemu mzee said ambaye pia hadi mauti yanamkuta alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, atakumbukwa zaidi na wadau wa soka kwa kuwa alikuwa mmoja wa watu waliobua vipaji vya soka kwa kuandaa mashindano mbalimbali yakiwepo ya Uhai.
Naye rais wa TFF Jamal Malinzi amesema kuwa katika Shirikisho lake amepoteza mtu mhimu ambaye alikuwa nguzo kubwa ndani ya TFF aliyekubali kukaa na watu wa rika lolote kwa ajili ya kujadili masuala ya soka , huku akimkumbuka kwa kuwa mmoja wa watu waliounganisha TFF na Azam kupta udhamini wa timu za vijana ikiwepo timu ya Taifa ya Vijana.
No comments:
Post a Comment