BREAKING

Tuesday 15 November 2016

SERIKALI YAKABIDHI BENDERA KWA MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA KUMSAKA MREMBO WA AFRIKA YATAKAYOFANYIKA NOVEMBA 26 NCHINI NIGERIA


Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape nnauye, amemkabidhi bendera ya taifa mrembo,Julitha Kabete kwa ajili ya kwenda kushiriki shindano la Miss Afrika mjini Calabar nchini Nigeria ambalo litafanyika Novemba 26 Mwaka huu.

Waziri Nape amekabidhi bendera hiyo huku akitoa nasaha kwa mrembo huyo kuwa na nidhamu katika shindano hilo ambalo ni kwa mara ya kwanza kufanyika, ambapo pia ametumia muda huo kumweleza kwamba Serikali ipo bega kwa bega na ushiriki wake kwani kwa sasa Serikali inatumia mashindano kama hayo kutangaza sanaa zaidi.

Aidha Waziri huyo amesema kuwa wanathamini warembo kwa kuwa wamekuwa wakitangza Tanzani kupitia shindano hilo ambalo kidunia lina umaarufu mkubwa hivyo watanzania wanapaswa kumpigia kura nyingi mrembo huyo, huku Julietha akisema kuwa atatumia vyema ushindani wake kwani iwapo atashinda atakuwa ameitangza kwa kiasi kikubwa Tanzania kupitia sanaa ya Urembo.

Kauli ambayo imeenda sambamba na ya Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga, kuwa katika mashindano hayo mrembo atakayepatikana atakuwa mwakilishi wa utunzaji wa Mazingira kufutia mabadiliko ya Tabia nchi.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube