Msanii wa Vichekesho Joti kati kati akitmbulishwa kuwa Balozi wa kifurushi cha DSTV Bomba,anayefuatia kushoto ni Meneja Uendeshaji wa DSTV Ronald Baraka Shelukindo ,wakwanza kulia ni Meneja Masoko Multichoice Alpha Joseph,.
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Ronald Baraka Shelukindo,akizungumzia punguzo wa Kifurushi cha DSTV Bomba
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Ronald Baraka Shelukindo,akizungumzia punguzo wa Kifurushi cha DSTV Bomba
Kampuni ya Multichoice Tanzania imetoa zawadi kwa wateja wake kuelekea kwenye msimu wa sikukuu ya Krismasi, baada ya kupunguza bei za vifurushi vyake pamoja na kuongeza channel kwenye kifurushi cha DSTV Bomba ambacho sasa mteja atalipia shilingi elfu kumi na tisa na miatisa sabini na tano.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Ronald Baraka shelukindo amesema kuwa wateja wao wataendelea kupata burudani kambambe hususani wapenzi wa soka pamoja na filamu kwa kuwa zitakuwa kwenye kifurushi cha DSTV Bomba, kupitia channel zake za Super Sport 12 na Supersport 4 ambapo Ligi ya Hispania itaonekana yote zaidi ya mechi 100.
Wakati huo huo Shelukindo pamoja na Meneja Mkuu wa Masoko wa DSTV Alpha Joseph, wamemtangaza msanii wa michekesho Lucas Mhavile, maarufu kwa jina la kisanii JOTI, kuwa balozi wake wa kifurushi cha DSTV Bomba kwa miezi sita,ambaye atasaidia kutangaza kifurushi hicho.
No comments:
Post a Comment