Ezi za Mwambete akiwa na miguu yake kabla ya Mguu mmoja kukatwa
Aliyekaa kitandani ni msukuma Kandanda wa zamani Athur Mwambete, na pembeni yake ni madaktari bingwa wanaomhudumia wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Professa Mohamed Janabi.
Na Said Makala
Wadau wa michezo kote nchini wameombwa kujitokeza kumsaidia mwana michezo Athur Mwambeta aliyelazwa katika taasisi ya magonjwa ya moyo ya Muhimbili.
Msaada mkubwa zaidi anaohitaji ni pesa ya kununulia miguu ya bandia.
Mtandao wako wa Shamakala360 ulimtembelea Athur na nikufanya naye mazungumzo,
Msomaji umuonaye hapo ni mchezaji wa zamani wa timu za soka za Sunderland na Simba, Athur Mwambeta ambaye jina lake kamwe si geni masikioni mwa familia ya wapenda michezo kutokana na umahiri wake katika kusakata kabumbu kuanzia miaka ya sitini na sabini.
Lakini tunavyozungumza hivi sasa hali yake si nzuri na amelazwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya taifa ya muhimbili jijini Dar es Salaam kufuatia maradhi ya miguu kuuma sana.
Mwambeta ambaye sasa anakabiliana na maradhi hayo kwa mara ya pili baada kuwa na hali katika cha hivi karibuni jambo lililopelekea kukatwa mguu wa mmoja.
Na i hivi sasa kufuatia athari katika mguu uliosalia kuendelea kuwa kubwa kuna uwezekano akapoteza tena mguu mwingine.
Hospitalini hapo nimefanikiwa kuzungumza na Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Professa Mohamed Janabi, ambapo alibainisha maendeleo ya Mwambeta hospitalini hapo,kuendelea vyema kupata matibabu lakinmi akitanabaisha kwamba anahitaji matibabu ya hali na mali na msaada mkubwa hususani miguu ya bandia ambayo mguu moja unauzwa milioni 20.
No comments:
Post a Comment