BREAKING

Friday 19 February 2016

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NAPE NNAUYE AMETENGUA RASMI UTEUZI WA KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA MICHEZO NCHINI HENRY LIHAYA KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA KIPINDI CHA MIAKA SABA



 Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya,ambaye ametenguliwa kuwa Mtendaji BMT


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, wakati alipozuru BMT,kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya,ambaye ametenguliwa BMT





 Na Said Makala


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye  ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Waziri Nnauye alitengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.

Nape ameongeza kwamba Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo.

Amesema  kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.

Kutokana na utenguzi huo Nape amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.

Vilevile,amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini.

Akihitimisha kauli zake Nnauye amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.




No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube