BREAKING

Tuesday 2 February 2016

MRADI WA GESI WA SONGOSONGO SERIKALI YAELEZEA MATUMAINI YA KUKAMILIKA IFIKAPO FEBRUARI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  JUSTIN NTALIKWA -Akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pan Africa Bwana David Robert wakati alipotembelea mradi wa uchimbaji wa visima vya Gesi.Songo Songo Mkoani Lindi

 Mkurugenzi wa Pan African David Robert akimwonyesha Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa,moja ya Visima vya Gesi vinavyotengenezwa




 Moja ya Mitambo inayo Chimba Visima vya Gesi-Songo Songo

 Mwandishi Said Makala

Serikali  imesema imeridhishwa na mradi wa gesi wa Songosongo ulioanza uzalishaji wake mwaka 2004 ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 10 mwaka huu kwa visima 12 vya gesi kukamilika.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa visima vya gesi wilayani Kilwa mkoani Lindi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa  amesema Serikali inaridhishwa na mwenendo wa uchimbaji wa visima vya gesi asilia unavyoendelea na anaamini itakuwa na faida kwa watanzania wote.

Amesema kuwa amefurahishwa na mwendendo wa ujenzi wa visima hivyo vya gesi ambapo amewataka waendesha mradi huo  Kampuni ya Pan African Energy wanaoendesha mradi huo wa uchimbaji wa visima vya gesi, kukamilisha haraka visima vilivyobaki

Kwa upande wake Meneja Operesheni wa Kampuni ya Pan African Energy ambao wanaendesha mradi huo wa uchimbaji wa visima vya gesi, Onestus Mujemula amesema hadi sasa wamekamilisha uchimbaji wa visima saba vinavyofanya kazi kati ya 12, ambapo amemweleza Katibu Mkuu huyo kuwa wapo katika utendaji mzuri wa kila siku ili kuhakikisha uzalishaji wa gesi katika visima vilivyosalia unakamilika.

 Aidha Katibu Mkuu huyo amepokea taarifa kuwa tayari visima saba vya gesi vimekamilika na vinafanya kazi na vinazalisha gesi futi za ujazo 150 na hadi kufikia Februari 10 mwaka huu mradi huo utakuwa umekamilika na kufikia visima vinavyofanya kazi 12 vitakavyokuwa vinazalisha futi za ujazo 200 kwa siku, huku akieleza kuwa hadi sasa zimetumika jumla ya dola milioni 67 katika uchimbaji wa visima vinne.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube