Msanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya kutoka Nchini Nigeria , Seyi Shay amesema anavutiwa na Tanzania inavyokua kisanaa licha ya kwamba bado wasanii wengi wanapaswa kujituma zaidi.
Nyota huyo ambaye anatamba na nyimbo yake ya 'Right Now' na video yake hiyo amesema hayo alipofanya mahojiano na waandishi wa habari katika chakula cha jioni Jijini Dar es salaam, chakula hicho ambacho kilindaliwa na kampuni ya Pepsi ambayo yeye ni Balozi ukanda wa Afrika.
No comments:
Post a Comment