Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete azindua rasmi jengo la Ofisi ya CCM, Wilaya ya Kibaha Mjini mkoa wa Pwani jana. Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa fedha za familia ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Slyvester Koka (kulia).
Mbunge wa Kibaha Mjini Slyvester Koka akieleza kuhusu mradi wa ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mjini mjini mkoa wa Pwani, kabla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuzindua jengo hilo
Viongozi wa CCM, Wilaya ya Kibaha mjini wakimkabidhi zawadi ya picha yake ya kuchorwa, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kabla ya kutoa vyeti kwa wana CCM mbalimbali walioshiriki kwa namna moja au nyingine kuimarisha Chama..
Zifuatazo ni mfululizo wa taswira mbalimbali alivyokuwa akionekana Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipohutubia wana CCM na wananchi kwa jumla baada ya kufungua Ofisi hiyo ya CCM Wilaya ya Kibaha mjini.. Kikwete alisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa hatua waliookisaliti chama wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, lakini akaonya hatua kuchukuliwa kwa uangalifu ili wasije wakachukuliwa hatua kwa kupakaziwa wanachama au viongozi ambao kwa kuonekana ni wanaonekana tu kuwa kkwazo kwa wenaotaka nafasi katika uchaguzi ujao.
Pia Mwekyekiti aliwataka WanaCCM kuzingatia ujenzi wa Uhai wa Chama kwa kuingiza wanachama wapya, kufanya vikao na pia kufanya maamuzi kwa busara
Aidha Kikwete akikana kuhusika kwa namna yoyote kutoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha, kuufuta uchaguzi uliopita. SASA ENDELEA KUPEZUI PICHA
No comments:
Post a Comment