JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais waJamhuri ya Guinea
Bissau Mheshimiwa Jose' Mario Vaz amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi hiyo itaendelea kushirikiana na
Tanzania katika nyanja mbalimbali, hususani katika uchumi kwa manufaa ya
wananchi wa nchi zote mbili.
Rais Jose' Mario
Vaz amesema hayo katika ujumbe wa barua uliwasilishwa kwa Rais Magufuli na
Mjumbe maalum wa Rais huyo Jenerali Omar Embalo, Ikulu Jijini Dar es salaam leo
tarehe 25 Februari, 2016.
"Napenda
kusisitiza kuwa nchi zetu ni marafiki wa muda mrefu, naomba urafiki na
mahusiano haya mazuri yaendelee na ninakuhakikishia kuwa nchi yangu itaendelea
kuuenzi ushirikiano huu" Ilieleza sehemu ya
ujumbe huo.
Aidha, Rais Jose
Mario Vaz amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuiongoza Tanzania
katika awamu ya tano na amemualika kuitembelea nchi ya Guinea Bissau ili
kuimarisha zaidi Uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake
Rais Magufuli amemshukuru Rais Jose Mario Vaz kwa kumtuma mjumbe maalum kwa
ajili ya kumletea ujumbe wa pongezi, na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea
kushirikiana na Guinea Bissau.
"Nakushukuru sana Jenerali Umaro Sissoco Embalo
kwa kuniletea ujumbe wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau na nakuomba
umwambie namshukuru kwa pongezi, mimi na serikali yangu tupo tayari kuimarisha
uhusiano na ushirikiano na Guinea Bissau ili mataifa yetu yaweze kunufaika
zaidi"Alisema Rais Magufuli
Wakati huo huo,
Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Ikulu Jijini Dar es salaam
leo.
Gerson
Msigwa,
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
25 Februari,
2016
No comments:
Post a Comment