Shirika la TAFEYOCO (Tanzania Feminist and Youth Change Organization) linalojihusisha na maswala ya Wanawake na vijana katika kutatua changamoto zao kiuchumi, kisiasa na kijamii limemuomba Mhe Rais apange muda wa kuonana na vijana wa mkoa wa Dar es salaam kama alivyofanya kwa wazee.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam mapema leo Februari 18, vijana hao kupitia Mwenyekiti wao Elvice John Makumbo wamebainisha kuwa miaka yote viongozi wa nchi ukutana na wazee na kusikiliza changamoto zao lakini kwa sasa Tanzania idadi kubwa ya watu ni vijana na ndio waliokuwa wanakesha na kuyalilia mabadiriko haya tunayoyaona kipindi hiki hivyo tunamuomba Mhe Rais akutane na vijana na kusikiliza changamoto zao na ushauri kwenye utendaji wake.
Tazama hapa kupitia
Mwenyekiti wa Shirika la TAFEYOCO, Elvice John Makumbo akiongea na wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment