Tazama video hapa:
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento akizungumza katika mkutano huo leo Feb 25.
Wadau wa kilimo wakifuatilia mkutano huo ..
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento akizungumza katika mkutano huo. Kulia kwake ni Profesa wa chuo cha Sheria, Arizona, Dale Beck Furnsh
Ofisa mahusiano wa wateja wadogo na wa Kati kutoka benki ya CRDB, Bi. Rehema Shambwe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Kongamano
la siku tatu juu ya sera ya kilimo linalotarajia kufikia tamati leo
Februari 25.2016 huku likiwa limeshirikisha wadau wa kilimo Zaidi ya
150, kutoka ndani ya nje ya Tanzania wametoa maoni yao mbalimbali namna
ya kuboresha kilimo hapa nchini ilikufikia maendeleo makubwa.
Kongamano
hilo lililokuwa na kauli mbiu: “Mabadiliko ya sekta ya kilimo na
mchango wake katika kukuza usalama wa chakula na lishe, kupunguza
umasini na kuleta ajira’ limefanyika jijini Dar es Salaam ambapo wadau
hao wameweza kutoa maoni yao hayo ikiwemo namna ya kufikia wakulima kwa
njia teknolojia ya mawasiliano.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd,
Bw. Freddie Manento amebainisha kuwa masuala ya teknolojia na
mawasiliano yanarahisisha upatikanaji wa habari mbalimbali ikiwemo
Kilimo ambapo kampuni yake imeamua kurahisha mpango huo ilikumfikia kila
Mtanzania ikiwemo hata yule wa hali ya chini kupitia mawasiliano na
fursa za kupata taarifa sahihi.
Amebainisha
kuwa, wakulima wanahitaji kupatiwa taarifa muhimu mbalimbali hivyo wao
wameweza kuboresha huduma za teknolojia ya kufikisha habari hizo kupitia
mpango wa Push for Change, ambao Mkulima kupitia simu yake hata kama ni
ya kawaida anaweza kupata habari za kina juu ya masoko na namna ya
kuwezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika.
Progamu
ya Push For Change inatoa taarifa mbalimbali hivyo kuwa msaada mkubwa
kw sekta ya kilimo. Huduma hyo pia wakulima na watu wengine wanaweza
kuipata kwa kujiunga na huduma hiyo, kwa kutuma neno Change kwenda namba
15774 na kuchagua huduma unayotaka ikiwemo kupata taarifa kama Kilimo,
Uchumi, biashara, afya, michezo na burudani, savei, elimu, utaliii na
nyinginezo.
Aidha,
kwa upande wake, Ofisa mahusiano wa wateja wadogo na wa Kati kutoka
benki ya CRDB, Bi. Rehema Shambwe amebainisha kuwa wamekuwa wakitoa
mikopo na ushauri kwa wakulima mbalimbali huku changamoto kubwa ni suala
la mitaji kwa wengi wa wakulima hao.
Bi.
Rehema Shambwe amewataka wadau na Serikali kuangalia namna ya kuweza
kuboresha bidhaa zinazotoka Tanzania ilikuweza kuhimili masoko ya
Kimataifa.
No comments:
Post a Comment