Meneja
wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama
barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin,
(katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya
Go4school, Henning Nathow.
Katika
kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi
jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na
Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada
wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.
Akizungumzia
msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa
lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule
ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara.
Alivitaja
vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha alama za
kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke, makoti yanayowatambulisha
waongozaji, kofia za kuwazuia na jua na mipira ya michezo mashuleni na
watatoa elimu katika shule hizo ili kuwasaidia watoto kujua sheria za
barabarani.
“Tumeamua
kutoa msaada huu kwa shule 18 na tutatoa elimu na tutakabidhi vifaa …
tunaamini msaada huu utaweza kuwasaidia watoto hao na tunaamini
itasaidia kupunguza ajali barabarani,” alisema Bi. Tharaia.
Akipokea
vifaa hiyvo kwa niaba ya Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter alisema
wanaishukuru CFAO Motors Group kwa kutambua umuhimu wa elimu na kutoa
vifaa vitakavyoweza kusaidia kuongoza wanafunzi wavukapo barabara.
“Tunashukuru
sana kwa msaada huu na mmeonyesha ni jinsi gani mnatambua umuhimu wa
elimu na sisi tupo pamoja nanyi na tupo tayari kupokea elimu hiyo,”
alisema Bi. Helen.
Alizitaja
baadhi ya shule ambazo zitapata vifaa hivyo kuwa ni Shule ya Msingi
Msimbazi, Boma, Mnazi Mmoja, Uhuru Mchanganyiko, Tabata, Ilala, Lumumba,
Muhimbili, Buguruni, Kasulu, Mkoani, Msimbazi Mseto, Hekima, Amana,
Mtendeni, Buguruni Viziwi na Tabata Jeta na Mtandani.
Pamoja
na hayo pia kunataraji kufanyika mashindano ya mbio za magari yaliyo na
lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya
CFAO Motors Group yanayofanyika nchini na yanataraji kumalizikia nchini
Rwanda.
Meneja
Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah (kulia) akionyesha
baadhi vifaa hivyo vya usalama barabarani kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani).
Mbio
hizo za kusaidia elimu nchini Rwanda zimepewa jina la The go4school
Charity Rally ambazo zimeshirikisha magari 18 ambayo yameanzia jijini
Dar es Salaam na yanataraji kufikia kilele chake Machi, 13 nchini Rwanda
na yatapita katika nchi za Kenya na Uganda na kisha Rwanda.
Akizungumzia
mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin
alisema mbio hizo za magari zimeanzishwa na taasisi ya Volkswagen kwa
kushirikiana na taasisi ya Opportunity International Germany kwa
kutambua kwao umuhimu wa elimu na usalama wa watoto wawapo barabarani.
Alisema
kuwa wamekuwa wakisaidia zaidi katika sekta ya elimu na sio mara ya
kwanza kufanya mbio hizo za magari kwani mwaka 2013 walifanya mbio kama
hizo kutokea Senegal hadi Ghana na mwaka 2015 walifanya kutokea Namibia
hadi Malawi na mara zote kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa ikihusika
kufanikisha mbio hizo.
Mwanzilishi
wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning Nathow (wa pili
kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia upatikanaji wa elimu
bora kupitia mradi wa go4school.
“Mbio
hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na hii sio
mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika na sisi
kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity International
Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,” alisema Potin.
Nae
Henning Nathow ambaye ndiyo mwanzilishi wa mradi wa go4school ulio na
lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu bora alisema wanafurahi kufanya
mbiao hizo ambazo zina lengo la kusaidia elimu nchini Rwanda wa
wanaamini elimu ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia kupambana na
umasikini.
Alisema
wanataraji kufanya mbio hizo na baada ya kufika Rwanda watayakabidhi
magari yanayotumika kwa ofisi za CFAO za Rwanda na baada ya hapo
watayauza na mapato yatakayopatikana watayakabidhi kwa serikali ya
Rwanda ili kusaidia sekta ya elimu.
“Elimu
ni njia ambayo inaweza kusaidia kumaliza janga la umasikini na sisi
tuna furaha kufanya mbio hizo kuelekea Rwanda ili kusaidia kupatikana
kwa elimu bora Rwanda,” alisema Nathow.
Afisa
Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya CFAO
Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa shule
18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto) akimkabidhi
Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter (wa kwanza
kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia wanafunzi
wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia) na
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
MAJALIWA APOKEA MISAADA WILAYANI RUANGWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa
ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya HUAWEI ya China , kijijini
hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan
Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa
Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze
kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja
wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa ma Mwanaidi Mussa na Mkussa Lukoloma (kushoto) wote wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwabaada ya kuwakabidhi kadi zao za bima ya
Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel iliyochangia
shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa kijiji hicho kufaidi huduma
za Bima ya Afya, Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment