BREAKING

Wednesday 24 February 2016

MKALI WA NDONDI THOMAS MASHALI KUTAFUTIWA MBABE PASAKA

Bondia Salum Nassoro akipasha na kocha wake, Maneno Abdallah katika gym yao iliyopo Mazense Midizini.
Promota wa mchezo huo, Haruna Musa katika picha ya pamoja na bondia, Salum Nassoro.
...........................................................................................................
Kampuni ya Dippo Boxing Promotion ya jijini Dar inayoongozwa na promota, Haruna
Musa imeandaa pambano la Uzito wa Kati ‘Middle Weight’ kati ya bondia Salum Nassoro wa Dar na Benson Mwakyembe wa Ruvuma mchezo utakaopigwa Siku Kuu ya Pasaka, Machi 28 mwaka huu.
Pambano hilo la kukata na shoka litapigwa kwenye uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma ambapo kwa mujibu wa promota huyo alisema kuwa mshindi wa siku hiyo atazichapa na bingwa wa Afrika ‘WBF, Thomas Mashali.
Mabondia hao ambao kila mmoja alitamba kumchapa mwenzake, waliwataka mashabiki
wa ndondi kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo ili waone ladha ya ndondi ya asili.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube