BREAKING

Thursday 30 July 2015

WAZIRI MKUU STAAFU MH EDWARD LOWASA AKIWA KATIKA PICHA MBALIMBALI ALIPOWASILI MAKAO MAKUU YA CHAMA CHA CHADEMA.

 Baadhi ya wananchi waliofurika kumlaki Lowasa. 

LOWASA ACHUKUA FOMU YA UGOMBEA URAIS CHADEMA.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa, akiwasili makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHAMADEMA, kachukua fomu ya kugombea Urais kupitia Chama hicho. 

KUELEKEA MSIMU MPYA WA LIGA KUU YA UINGEREZA MULTICHOICE, TANZANIA KUZINDUA MSIMU MPYA WA LIGA KUU YA ENGLAND

 Meneja Masoko wa DSTV Furaha Samalu , akizungumzia uzinduzi huo, wengine ni Barbara Kabongi Meneja Uhusiano na wa mwisho kulia ni Baraka Shelukindo, Meneja uendeshaji DSTV. 

NISHATI YA GESI ASILIA KUTUA DAR MWEZI UJAO

Baadhi ya Mitaambo ya Gesi asilia

 

Jitihada za serikali katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa umeme nchini, sambamba na matumizi ya nishati ya gesi asilia, kwa ajili ya kufulia mitambo ya umeme hatimaye vimekamilika.

Kuanzia mwezi ujao uzalishaji umeme kwenye mradi wa Kinyerezi jijini Dar es salaam utaanza kuzalisha megawati 75 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya taifa, baada ya kukamilika kwa asilimia 95 ya mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha megawati 150.

Wajumbe wa bodi ya shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC wakitembelea miradi ya uzalishaji na uchakataji wa gesi kwenye kiwanda cha Gesi Songosongo pamoja na mitambo ya kufua umeme wa gesi wa Kinyerezi na Tegeta wameelezea kuridhishwa na hatua zilizofikiwa kwenye miradi hiyo iliyoghrami taifa zaidi ya shilingi trilion mbili.

Kuhusiana na kukamilika kwa mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi wenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 150, meneja wa Tanesco toka Mradi wa Kinyerezi 1 anaeleza zaidi.

Mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni wa pili kumilikiwa na Serikali kupitia TPDC kwa asilimia mia moja baada ule mradi wa bomba la gesi kutoka Ubungo mpaka maeneo ya Mikocheni uliozinduliwa tarehe 26 Julai, 2014.

EDWARD LOWASSA KUCHUKUA FOMU LEO YA URAIS KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa pamoja na Mkewe Regina Lowasa wakiwa wakionyesha  kadi zao baada ya kujiunga na Chama cha Demeokrasia na Maendeleo CHADEMA.


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa leo  anatarajiwa kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya wanachama wa Chadema kupeperusha bendera ya chama hicho kwa nafasi ya Urais.

Bw. Lowasa ambaye ameleta hamasa mpya katika siasa za Tanzania kutokana na uamuzi wake wa kuhamia chama cha upinzani, anatarajiwa kufika saa tano makao makuu ya chadema kwa ajili ya kuchukua fomu ya urais.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusiana na taarifa zilizoenea kwenye baadhi ya mitandao kuwa watendaji wakuu wa chadema inasadikiwa wamehama chama hicho kupinga uamuzi wa kumpokea Lowasa, Salum Mwalimu amefafanua kuwa Lowasa leo atachukua fomu hiyo

Tuesday 28 July 2015

LOWASA AJIUNGA NA CHADEMA

Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe, akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, wakati wa kumtambulisha kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

LOWASA AJIUNGA RASMI CHADEMA,UKAWA WASEMA WAMEPATA HAZINA, WAMSHUKURU KIKWETE....

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kumtambulisha kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambapo ametangaza kukihama Chama cha Mapinduzi CCM.

QUALITY GROUP WAZINDUA YADI KWA AJILI YA MAGARI YA CHEVROLET NA ISUZU




Monday 27 July 2015

BOBBI KRISTINA MTOTO WA WHITNEY AFARIKI DUNIA


Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.
Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.
Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''.
Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado.Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitliza kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufa.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.

UKAWA WAMSAFISHA LOWASA, WASEMA NI MSAFI ANAWAFAA, HANA KASHFA YA UFISADI

Khamis

Umoja wa Vyama Vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi -Ukawa vimemtaka na Waziri Mstaafu bw.Edward Lowasa kujiunga na Umoja huo na kuahidi kushirikiana nae katika kuhakikisha kuwa wanaleta magauzi na kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari jijini dsm Mwekiti mwenza wa Umoja huo James Mbatia amesema Umoja huo umetafakari na kutoa fursa kwa kila mtanzania mwenye kutaka mageuzi ajiunge na umoja huo ili waunganishe nguvu ya kukiondoa chama cha mapinduzi madarakani.

Kutokana na Tamko hilo waandishi wa habari waliokuwapo katika mkutano huo walitaka ufafanuzi Juu ya kumkaribisha Bwana Lowasa huku viongozi hao awali walikuwa wakimshutumu kuhusika na Ufisadi katika sakata la Richmond na kusababisha kujiuzuru kwake.

M/kiti mwenza wa Ukawa Prof.Ibrahim Lipumba amesema Tatizo la Ufisadi alilotuhumiwa Bw.Lowasa linatokana na Mfumo uliopo katika Chama cha mapinduzi na Serikalini .

Aidha Waandshi wa habari pia walitaka kujua kuhusu nafasi ya Ugombea Urais Kupitia umoja huo ikiwa Lowasa atakubali kujiunga nao Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa  Emmanuel  Makaidi anaeleza...

Hata hivyo Prof.Lipumba amesema Suala na Mgombea Urais kuchelewa kutangazwa linatokana na marekebisho na makubaliano ndani ya vyama husika na Umoja huo lakini akaweka wazi kuwa mgombea urais kupitia Umoja huo atatangazwa kabla ya tarehe moja mwezi  agosti .


Mwekiti mwenza wa Umoja huo James Mbatia akitoa tamko hilo,la kumkaribisha Lowasa mbele ya waandishi wa habari jijini dsm

LOWASA AKUTANA NA VIONGOZI WA UKAWA, ATANGAZWA RASMI KUJIUNGA NAO.




Friday 24 July 2015

TTCL YAUNGANISHA OFISI NA KANDA ZA MSD KWENYE MKONGO

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha orodha ya wateja wanaopata huduma ya mkongo toka kampuni hiyo kwenye tableti yake, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL kwenye hafla ya kukabidhi mradi wa huduma ya mkongo kwa Bohari ya Dawa nchini (MSD) leo jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akionesha orodha ya wateja wanaopata huduma ya mkongo toka kampuni hiyo kwenye tableti yake, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL kwenye hafla ya kukabidhi mradi wa huduma ya mkongo kwa Bohari ya Dawa nchini (MSD) leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.

UJUMBE WA MADAKTARI BINGWA WA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV WAWASILI BANDARI YA ZANZIBAR

Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Seif Suleman akiwa katika bandari ya Zanzibar kuupokea Ujumbe wa Madaktari kutoka Jumuiya ya Watanzania Washington ukiwa wenyeji wa PBZ na Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora Zanzibar wakiwa katika bandari hiyo kuupokea kwa ajili ya kutoa huduma ya Afya kwa Wananchi wa Zanzibar katika hospitali ya Mnazi mmoja kesho, Kwa muji wa Mkurugenzi wa Idara hiyo Ndg Adila Hilal Vuai amesema utatoa huduma ya Uchunguzi wa Satatani ya Maziwa kwa Kinamama, Kisukari, Presha Meno na tiba nyengine kwa wananchi wa Zanzibar watakaofika katika hospitali hiyo kupata huduma hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa PBZ Ndg Seif Suleiman akisalimiana na mmoja wa madaktari hao Bingwa walipowasili katika bandari ya forodhani wakitokea Dar -es- Salaam walikuwa wakitowa huduma hizo kwa Wananchi.katikati Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Ndg Adila Hilal Vuai. wakiwapokea wageni wao.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washington Ndg Iddi Sandaly akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBA) Ndg Seif Suleiman alipowasili katika bandari ya Zanzibar wakitikea Dar na Ujumbe wa Madaktari 17 watakuwa Zanzibar kwa kutoa huduma ya Tiba kwa Wananchi wa Zanzibar katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kesho asubuhi.

KADAMA MALUNDE ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA WANAHABARI SHINYANGA

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo. Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo. Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC)

HUDUMA YA UPASUAJI WA WATOTO WENYE UGONJWA WA KICHWA KUJAA MAJI NA MGONGO WAZI YAZINDULIWA RASMI KATIKA HOSPITARI YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA


Na Faustine Ruta, Bukoba

Shirika lisilokuwa la serikali la Friends of Children with Cancer Tanzania (FOCC TZ) lazindua rasmi huduma ya upasuaji wa watoto wenye ugonjwa wa vichwa kujaa maji na mgongo wazi mkoani Kagera katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa ambapo jumla ya watoto arobaini wenye tatizo hilo wanatajiwa kufanyiwa upasuaji kuanzia Julai 25-26, 2015. 

Mkurugenzi wa shirika la FOCCTZ Bw. Walter Miya katika uzinduzi huo alisema kuwa baada ya kutoa matangazo kupitia redio za jamii mkoani Kagera kwa muda wa siku mbili wameweza kupata watoto 70 wenye tatizo la vichwa kujaa maji na mgongio wazi kutoka katika wilaya zote saba za mkao wa Kagera na nje ya mkoa. Bw. Walter alisema watoto walioweza kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa msaada wa shirika lake ni 40 na watoto 30 wameshindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwasafirisha watoto hao, pia changamoto ya wananchi kuwa na imani potofu ya kuwa watoto hao wamerogwa

Huduma hiyo inatolewa mkoani Kagera na shirika la Friends of Children with Cancer Tanzania wakishirikiana na Madaktari wataalam wa upasuaji huo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando pia kutoka katika kitengo cha Muhimbili Orthopaedic Instutite (MOI) kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Taifa Muhimbili. 



UJIO WA RAIS WA MAREKAN BARACK OBAMA NCHINI KENYA, ULINZI MKUBWA WAIMARISHWA.













MAELUFU YA WANANCHI WAKIMSIKILIZA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM JOHN POMBE MAGUFULI

 Magufuli akihutubia wananchi.



Wednesday 22 July 2015

JOSEPHINE MICHAEL MGAZA, ALIVYOJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE VITI MAALUM MKOA WA TANGA, AJA NA MATUMAINI KIBAO.




MAGUFULI ASIMAMISHA SHUGHULI KWA MUDA, KAHAMA WANANCHI WAJITOKEZA KUMLAKI...

 Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM, akisaini moja ya Vitabu, vya Ofisi za chama hicho kablya kuwahutubia wananchi.
 Wananchi wa Kahama wakiwa wamefurika katika Mkutano wakati alipokuwa akiwasalimia.

 Magufuli akingumza na wananchi wa Kahama.
MGOMBEA Urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, John Pombe Magufuli, anaendelea kujitambulisha katika Mikoa ya kanda ya Ziwa ambapo leo alikuwa katika Mkoa wa Kahama nakulakiwa na wananchi wengi.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube