Kwa mara nyignine tena watanzania wamepata uhakika wa kushuhudia michuano mbalimbali mikubwa ya kimataifa baada ya DStv Kupitia
SuperSport
kuingia makubaliano ya kurusha michuano mikubwa ya kimataifa,
ikiwemo michuano ya
UEFA Euro 2020
pamoja na ile ya kufuzu
UEFA Euro 2020
na pia michuano ya ulaya ya kufuzu kombe la dunia
2022
nchini Qatar.
Pia kuna lulu nyingine kwa watazamaji wa DStv hasa washabiki wa kandanda kwani pia mashindano mapya ya Ligi ya UEFA itakayoshindaniwa na timu kutoka nchi zote 55 ambazo ni wanachama wa UEFA. Michuano hii pia itakuwa ikionyeshwa katika chaneli ya SuperSport.
Makubaliano haya yanawahakikishia watazamaji wa DStv kushuhudia michuano yote mikubwa ya soka kila msimu hadi mwaka 2022.
“UEFA inafurahi kuendelea na kuimarisha uhusiano wake wa muda mrefu na supersport” amekaririwa Guy-Laurent Epstein, Mkurugenzi Mtendaji wa UEFA Events SA. “Supersport ni mshirika wa miaka nenda rudi wa UEFA na tunaimani kubwa kuwa SuperSport itaendelea kuwahakikishia watazamaji matangazo ya kiwango cha juu na pia amsha amsha ya UEFA 2018-2022 kwa mamilioni ya watazamaji wa mitandange hiyo barani Afrika – Kusini mwa jangwa la Sahara.
UEFA Euro 2020, ni moja ya michuano itakayokuwa na shamrashamra nyingi ikizingatiwa kuwa itakuwa inatimiza miaka 60 tangu kuanza kwa michuano hiyo. Michuano hiyo itafanyika katika miji 13 ya nchi 13 tofauti barani Ulaya.
Michuano ya kufuzu ya Ulaya (The European qualifiers) itakuwa ya aina yake wakati ambapo nchi 55 zitakabana koo kuwania nafasi 24 za kushiriki michuano hiyo. Michuano hii ya kufuzu itaanza March 2019 hadi March 2020.
“Hii ni mikataba mikubwa na muhimu sana” amesema Gideon Khobane, Afisa Mkuu wa SuperSport. “Michuano ya Ulaya kwa kawaida huwa na mvuto mkubwa sana kwa watazamaji wetu hivyo kuyafanya moja ya mashindano muhimu sanan. Tunaamini kuwa michuano hii inaendelea kuwa mikubwa na maarufu Zaidi hivyo bila shaka ushirikiano wa Supersport na UEFA utaongeza chachu katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment