Ligi ya Mkoa mpira wa wavu imeendelea leo katika Uwanja wa taifa wa ndani jijini Dar es Salaam, ambpo timu ya CDS VC imeumana vikali na timu ya Tanzania Prisons.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano wa chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam Nasroro Sharif,amezungumzia mashindano hayo ambayo yamekuwa maarufu sasa, huku akijivunia wingi wa mashabiki waliofika kuzishangilia timu zao, jambo ambalo hata yeye limemtia moyo kwani awali michuano hiyo ilikuwa haina mashabiki wengi kiasi hicho.
Amesema mwitikio huo wa mashabiki ni inshara kuwa mchezo huo sasa una mvuto mkubwa na ndio chanzo cha kufikia mafanikio makubwa kiasi hicho.
Amesema michuano giyo ya Ligi Mkoa mwaka 2017 mzunguko wa pili umekuwa mgumu na wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kujiandaa vizuri.
No comments:
Post a Comment