BREAKING

Monday, 19 June 2017

POLEPOLE AFANYA MAZUNGUMZO UJUMBE KUTOKA KITUO CHA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI CHA UHOLANZI, OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CCM, DAR ES SALAAM, LEO


 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Meneja Mradi wa kushawishi Siasa Shirikishi katika kuimarisha vyama vya Siasa hapa nchini, hasa katika ushiriki wa Wanawake na Vijana katika masuala ya Siasa, unaoendeshwa na Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) kwa kushirikiana na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD),  Arjan Van Der Waal, wakati alipokutana na ujumbe wa Meneja huyo na Mwakilishi wa NIMD Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Watatu kulia ni Mwenyeji wa ugeni huo, Daniel Loyc kutoka TCD. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akimsalimia Mwakilishi wa Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) Kanda ya Afrika Dk. Augustine Magolowondo kutoka Malawi, alipopokea na kufanya mazungumzo na ugeni huo kutoka NIMD, leo
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiwakaribisha kuketi kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza na ujumbea kutoka Kituo cha Demokrasia ya Vyama Vingi cha Uholanzi (NIMD) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Katika Mazungumzo hayo, Polepole aliitaka NIMD kuja kufanya kazi nchini kwa lengo la kuinua hadhi ya siasa nchini badala ya kubomoa. "Hatutarajii NIMD ije kufanya mambo hasi, mradi usilenge kuondoa madarakani Chama tawala, bali uwe chachu katika kuhamasisha uungaji mkono mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dk. John Magufuli kama haya ya kulinda rasilimali za nchi", alisema Polepole. 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube