BREAKING

Tuesday 13 June 2017

YAMETIMIA - LIGI YA KIKAPU MAREKAN














Hatimaye Golden State Warrior wameshinda ubingwa wa ligi ya kikapu nchini Marekani baada ya kushinda mechi nne kati ya tano zilizokwishachezwa katika mfululizo wa mechi saba za fainali kuu ya ligi ya kikapu nchini Marekani.

Katika mechi ya tano ambayo ndiyo imeamua ubingwa kwa Warriors, imeisha wa Cleveland kukubali kipigo cha 120 kwa 129 na kuvuliwa rasmi ubingwa walioutwaa baada ya kuwashinda hao hao Warriors msimu uliopita.

Licha ya Lebron James kuibuka kidedea kwa kuwa na pointi nyingi zilizofika 41 zaidi ya yeyote kwenye mchezo huo, hazikuinusuru timu yake kufungwa na Warriors waliokuwa bado wanaugulia maumivu ya kufungwa msimu uliopita.

Kipekee Kevin Durant amefikia ndoto aliyowahi kuwa nayo, kwamba siku moja atwae ubingwa ambapo alieleza azma ya kuhamia Warriors ili apate nafasi ya kutwaa ubingwa, jitihada zake tangu msimu uanze, kwenye mechi za mtoano na hatimaye fainali kuu yyeye kuongoza kwa alama za kufunga na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.

Durant pia ameifikia rekodi ya kufunga wastani wa zaidi ya alama 30 na zaidi kila mechi katika mikutano mitano ya fainali kuu, rekodi ambayo imedumu miaka 17 tangu iwekwe na Shaquille O' Neal mwaka 2000.

Ubingwa huu kwa Warriors unakuwa ni wa pili katika kipindi cha misimu mitatu ya hivi karibuni baada ya kufanya hivyo mwaka 2017 kabla ya kupokwa mwaka 2016 na Cleveland na sasa wakiurejesha tena mwaka 2017.


Wachezaji wengine wa Warriors waliokuwa chachu ya ushindi katika fainali msimu huu, ni pamoja na Steven Curry, Draymmond Green, Andre Igodala na Zaza Pachulia.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube