BREAKING

Monday, 12 June 2017

WANAHARAKATI 42 KATI YA 50 WAFIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO KWA LENGO LA KUCHANGISHA FEDHA ZA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Wanaharakati walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro wakiimba na kucheza wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro.
Timu ya Wanaharakati 86 kutoka taasisi na kampuni mbalimbali walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia mapambano dhidi ya Ukimwi wakishuka kutoka katika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akijiandaa Timu ya  Wanaharakati wakati wakishuka kutoka kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zara ,Zainabu Ansel (katikati) akiowangoza wanaharakati hao wakati wakishuka katika lango la Mwika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Herman Kapufi aliyeshiriki Changamoto ya kupanda Mlima  Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira (kulia ) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Rombo ambaye ni kaimu Mkuu wa wilaya ya Moshi,Agnes Hokororo (katikati) na kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi ,Aisha Amour .
Baadhi ya Wanaharakati walioshiriki changamoto hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi ,TACAIDS ,Dkt Leonard Maboko akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea wanaharakati hao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitoa hotuba yake ya kwanza wakati w hafla fupi ya kuwapokea wanaharakati hao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita,Richard Jordnson mara baada ya kutoa hotuba yake.
Wawakilishi wa Benki ya NMB,wakiongozwa na Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi ,Emanuel Kishosha wakifuatilia hafla hiyo ,NMB ni moja kati ya taasisi zilizochangia katika kufanikisha wanaharakati kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitoa vyeti kwa wanaharakati 42 kati ya 50 waliopanda na kufanikiwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu ,Richard Jordnson akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Rombo,Agnes Hokororo ambaye pia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Moshi akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya wanaharakati walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi.
Kaimu mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Charles Ngendo akizungumza katika hafla hiyo. 

Wanaharakati katika changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi kupitia kampeni ya Kili Challange inayoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube